Wajumbe wa Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango, wametembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa zahanati mpya katika kijiji cha Lemugur Kata ya Mateves.
Mradi huo unatekelewa kwa gharama ya shilingi milioni 92.4 fedha kutoka Serikali kuu kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).
Katika ziara hiyo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Arusha, mhe. Dkt. ojung'u Salekwa lkwa niaba ya waheshimiwa madiwani wote wa halmashauri ya Arusha ameishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia TASAF kwa kutoa fedha kwaajili ya ujenzi wa Zahanati hiyo na kuwapongeza watalam wa halmashauri pamoja na kamati zote za ujenzi kwa kusimamia vyema matumizi sahihi ya fedha hiyo ya Serikali.
Zahanati hiyo itasaidia upatikaji wa huduma za matibabu kwa wananchi wa kijiji hicho kwa ukaribu zaidi na kuondoa adha iliyokuwepo hapo awali ya wananchi kutembea umbali mrefu kutafuta huduma za matibabu katika Vijiji jirani.
Akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi huo, Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Lemugur, John Sanin'go, amesema kuwa mbali na zahanati hiyo kutoa huduma kwa wananchi pindi itakapokamilika, lakini pia ujenzi wa zahanati hiyo umesaida kutoa ajira za muda mfupi kwa wakazi wa kijiji hicho ambazo zinasaidia kujipatia kipato kwaajili ya matumizi ya familia zao.
ARUSHA DC ni Yetu, Tushirikiane Kuijenga"
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.