Na. Elinipa Lupembe.
Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za mitaa, wamemuagiza Waziri, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, kujenga bweni la wavulana apmaoja na uzio kwenye shule ya sekondari Oldonyowas, halmashauri ya Arusha, wakati kamati hiyo ya Bunge, ilipotembelea shuleni hapo, kukagua miradi inayotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii - TASAF.
Wajumbe wa Kamati hiyo, wamefikia uamuzi huo baada ya kupokea maombi kutoka kwa wanafunzi, wazazi na viongozi wa kijiji na kata ya Oldonyowas, kutoa ombi kwa kamati hiyo, kujengewa bweni la wavulana na uzio wa shule, kutokana na wanafunzi wengi wanaosoma shuleni hapo, wanatoka kwenye familia za wafugaji, familia ambazo wana tabia ya huhama makazi yao, wakati wa ukame ili kufuata malisho ya mifugo yao, na kusababisha watoto wengi kuacha shule kufuata familia zao.
Akizungumza baada ya kukagua na kuridhishwa na utekelezaji wa miradi hiyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Utawala na Serikali za mitaa, Mheshimiwa Abdalah Kalembo, ameweka wazi kuwa, kamati hiiyo imeona umuhimu wa kujenga bweni la wanafunzi wavulana shuleni hapo, ili kuwapa wigo mpana na watoto hao kutika familia za wafugaji, kuwa na mazingira rafiki ya kusomea, tofauti na mazingira ya nyumbani ambayo familia zao huishi kwa kuhama hama.
"Kama alivyosema mheshimiwa Diwana wa Oldonyowas, watoto hawa wanatoka kwenye familia za wafugaji, isingekuwa kuna bweni hapa, watoto hawa wasingekuwepo shuleni hapa leo, wangehama na familia zao, ili kuhakikisha watoto wote wa familia za wafugaji wanapata haki ya kusoma, mheshimiwa Waziri, fanyeni utaratibu wa kujenga bweni la wavulana na uzio katika shule hii kwa haraka" amesisitiza Mwenyekiti wa Kamati Mheshimiwa Bulembo.
Hata hivyo, Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa, amekubali ombi na agizo hilo, na kusema kuwa, utaratibu wa kuanza ujenzi wa bweni la wavulana na uzio katika shule hiyo, utaanza mapema, kwa kuwa serikali ya awamu ya sita, imejipanga kupambana na adui ujinga kwa kuhakikisha watoto wanaotekea kwenye kaya zenye uhitaji, zinazohudumiwa na mradi wa TASAF zinapata elimu katika mazingira rafiki.
"Kupitia miradi ya TASAF serikali imejipanga kupambana na adui wa haki, anayesababishwa zaidi na ujinga, maradhi na umasikini, maadui hao wote wanaondolewa kupitia miradi ya TASAF, ujenzi wa bweni na uzio, utafanyika kwa haraka ili kunusuru watoto hawa wasiathirike katika masomo yao, kwa kuwa kipaumbeke cha serikali ni kuinua kipato cha kaya ambazo hazina uwezo, ili kuinua uchumi na ustawi wa kaya hizo" amesisitiza Waziri Mchengerwa.
Awali Diwani wa kata ya Oldonyowas, Mheshimiwa Kijana Saruni, licha ya kuishukuru serikali kwa kuona umuhimuwa wa wananchi wa watoto wa kijiji hicho kwa kuwapa miradi mingi ya TASAF, aliwasilisha mbele ya kamati hiyo ya Bunge, ombi la kupatiwa mradi wa ujenzi wa bweni la wavulana pamoja na uzio katika shule ya sekondari Oldonyowasi, kwa kuelezea matokeo yalionekana kwa muda mfupi kutokana na uwepo wa bweni la wasichana na kuongeza kuwa uwepo wa bweni la wavula utasaidia watoto wa jamii za kifugaji kusoma.
"Uwepo wa bweni la wasichana, umesaidia wanafunzi kuendelea na masomo, kungekuwa hakuna bweni, wanafunzi hawa wasingikuwepo shule leo wakati wa msimu wa ukame, watoto wengi wangekuwa wameondoka na wazazi wao, kwenda kutafuta malisho ya mifugo, tunaomba mtusaidie ujenzi wa bweni na kwa watoto wa kiume ili waweze kusoma kwa utulivu" amesisitiza Mheshimiwa Diwani.
Awali Kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za mitaa, imetembelea kijiji cha Oldonyowas, na kukagua miradi inayotekelezwa na TASAF awamu ya III, ikiwemo ujenzi wa jengo la utawala, vyumba vya madarasa, vyoo, nyumba mbili za walimu, mabweni mawaili ya wasichana,shule ya sekondari Oldonyowas, pamoja na mradi wa uhawilishaji fedha kwa kaya masikini na vikundi vya kuweka na kukopa.
Tangu mwaka 2014, TASAF awamu ya III na mpango wa kunusuru kaya masikini, imetekeleza katika vijiji 45 vya halmashauri ya Arusha na kuzifikia ya jumla ya kaya 9,107, huku kaya hizo zikipokea fedha kwa mizunguko 28 na jumla ya shilingi bilioni 9.5 zilihawilishwa kwa walengwa jumla ya miradi 46 yenye thamani ya shilingi bilioni 2.1 ilitekelezwa katika sekta ya elimu, afya, miundombinu ya barabara, uwezeshaji wananchi kiuchumi kupitia vikundi vya kilimo, ufugaji na utunzaji wa mazingira.
ARUSHA DC
KaziInaendelea✍✍
PICHA ZA MATUKIO YA ZIARA
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Utawala na Serikali za mitaa, wakikagua miradi ya miundombinu ya shule ya sekondari Oldonyowas, wakiongozwa na mwenyekiti wa kamati Mhe. Abdala Kalembo na Waziri OR Menejimenti ya Utmishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Mohamedi Mchengerwa, wakati wa ziara ya kamati hiyo, kukagua miradi inayotekelezwa na serikali kupitia TASAF awamu ya III.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Utawala na Serikali za mitaa, wakizungumza na wanafunzi wasichana wa shule ya sekondari Oldonyowas, wakati wa ziara ya kamati hiyo kijijini hapo kukagua miradi ya miundombinu ya shule ya sekondari Oldonyowas, wakiongozwa na mwenyekiti wa kamati Mhe. Abdala Kalembo na Waziri OR Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mhe. Mohamed Mchengerwa.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Utawala na Serikali za mitaa, Mheshimiwa Abdalah Kalembo, akizungumza na hadhara ya wananchi wa kijiji cha Oldonyowas, halmashauri ya Arusha, wakati wa ziara ya kukagua miradi inayotekelezwa na serikali kupitia Mfuko wa maendeleo ya Jamii - TASAF awamu ya III, katika shule ya sekondari Oldonyowas.
Waziri Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa, akizungumza na hadhara ya wananchi wa kijiji cha Oldonyowas, halmashauri ya Arusha, wakati wa ziara ya kukagua miradi inayotekelezwa na serikali kupitia Mfuko wa maendeleo ya Jamii - TASAF awamu ya III, katika shule ya sekondari Oldonyowas.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Utawala na Serikali za mitaa, wakikagua mradi wa mabweni ya wasichana shule ya sekondari Oldonyowas, wakati wa ziara ya kamati hiyo, kukagua miradi inayotekelezwa na serikali kupitia TASAF awamu ya III.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.