Wajumbe wa Kamati ya Siasa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Arumeru, wametembelea na kukagua miradi miwili ya ujenzi wa maabara na nyumba ya watumishi wa afya zahanati ya Bwawani.
Miradi yote miwili imeanza kwa kutekelezwa kwa nguvu za wananchi, ikiwa ni nyumba ya watumishi yenye sehemu ya kuishi familia mbili pamoja na jengo la maabara.
Wajumbe hao wameuagiza uongozi wa halmashauri kupeleka fedha za kukamilisha majengo hayo, kutokana na uhitaji mkubwa wa huduma za afya kwa wanachi wa eneo hilo.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Arumeru Noel Severe, amemuagiza mkurugezni wa halmashauri ya Arusha, kuona kuwa ukamilishaji wa jengo hilo kuwa kipaumbele na kufanyika hata kwa dharura, kutokana na hali halisi ya eneo hilo.
Aidha Mwenyekiti Severe, amewaponheza wanachi wa Bwawani kwa juhudi walizozionyesha katika kujieletea maendeleo yao, na kuwasistiza kuwa CCM inatambua na kuthamini kazi iliyofanyika na kwamba serikali itakamilisha majengo hayo ili kuwatia joto wananchi wa Bwawani.
"Sisi kama Chama, tuko nyuma yenu, tunatambua mchango na juhudi zenu wanabwawani zaidi tutahakikisha majengo haya yanakamilika, kwa kushitikiana na uongozi wa halmashauri ya Arusha sambamba na kuongeza idadi ya wahudumu wa afya". Amesisitiza Mwenyekiti huyo wa CCM
Hata hivyo, Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha, ameahidi kutekeleza agizo hilo na kufafanua kuwa kwa mwaka huu wa fedha tayari nyu,ba hiyo ilipelekewa shilingi milioni 10 ambazo zilitumika kukamilisha upande mmoja wa nyu,ba hiyo, huku wakijipanga kuleta fedha nyingine za kukamilisha sehemu ya pili ya nyumba hiyo.
Ziara hiyo ni maalumu kwa ajili ya ufuatiliaji wa utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2020 - 2025.
"ARUSHA DC ni Yetu, Tushirikiane Kuijenga"
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.