Na. Elinipa Lupembe.
Wajumbe wa Kamati ya Siasa mkoa wa Arusha wameridhishwa na utekelazaji wa miradi ya maendeleo, inayotekelezwa na fedha za Umma, katika halmashauri ya Arusha, wilaya ya Arumeru.
Wajumbe hao wameridhishwa na utekelezaji wa miradi hiyo, waliyokiri inabainisha ubora wa mradi kwa kulinganisha na thamani ya fedha iliyotumika, wakati wa ziara ya kutembelea miradi 8 yenye thamani ya shilingi milioni 914.3, katika sekta ya Elimu, Afya pamoja na miundombinu ya barabara, katika halmashauri ya Arusha mapema wiki hii..
Aidha Wajumbe hao wamefurahishwa zaidi na utekelezaji wa miradi ya maendeleo, inayotokana na fedha za mapato ya ndani ya halmashauri ya Arusha, ikiwemo mradi wa shule ya mchepuo wa kiingereza Enaboishu Academy, miradi ambayo imekamilika kwa wakati na kwa kuzingatia bajeti iliyotengwa na Serikali kwa mwaka husika.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mjumbe wa Kamati ya Siasa mkoa wa Arusha, Moloimet Olemoko amebainisha kuwa, Kamati hiyo ya Siasa, imeridhishwa na hali ya miradi yote iliyotembelewa na kuongeza kuwa hii ni kuonesha kazi nzuri inayofanywa na serikali ya awamu ya sita, inayoongozwa na mheshimiwa Rais mama Samia Suluhu Hassan.
"Miradi ni mizuri, imetekelezwa kwa viwango na ubora unaokubalika, imetekelezwa kwa kuzingatia Ilani ya Chama cha Mapinduzi pamoja na maenelekezo yanauotolewa na serikali, ikiwa na lengo la kuwahudumia watanzania wote bila kujali itikadi zao, tunaponheza sana juhudi za Mheshimiwa Rais, Mama yetu Samia" amesema Olemoko.
Naye mkuu wa wilaya ya Arumeru, Mhandisi Richard Ruyango amesema kuwa, utekelezaji wa miradi hiyo, unapambanua juhudi za serikali ya awamu ya sita kisekta, kwa kupanua wigo katika sekta ya elimu kwa kujenga vyumba vya madarasa pamoja na kuongeza vituo vya afya katika wilaya ya Arumeru.
Aidha amewataka walimu kuongeza bidii katika kazi ya kufundisha sambamba na kuwa wabunifu katika kuwafundisha wanafunzi, kwa kuwa taifa limejikita kipambana na adui ujinga, umaskini na maradhi hivyo, watoto wanapaswa kuwapata elimu bora itakayo likomboa taifa, zaidi amewaomba wananchi kutunza miundombinu iliyojengwa kwenye maeneo yao, ili iweze kutumiwa na vizazi vijavyo.
"Serikali ya awamu ya sita imewekeza fedha nyingi kwenye sekta ya Elimu ambapo Wilaya ya Arumeru imepata fedha za kujenga vyumba vya madarasa 170 pamoja na shilingi bilioni 2.4 za ujenzi wa miundombinu ya barabara, lengo likiwa ni kuboresha huduma za jamii katika wilaya yetu ya Arumeru" Amesisitiza Mkuu huyo wa Wilaya.
Hata hivyo, Mkuu wa shule ya Sekondari Kimnyaki, mwalimu, Paschal Ginana, ameishukuru serikali kwa kuwekeza nguvu nyingi kwenye sekta ya elimu, nguvu ambayo imewesha wanafunzi kujifunza katika mazingira bora huku walimu wakirahisishiwa tendo la kufundisha kupitia ubora wa vyumba hivyo vya madarasa.
Jumla ya miradi 8 yenye thamani ya shilingi milioni 914.3, imetembelewa na kamati hiyo ya siasa ikiwemo miradi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa, ujenzi wa shule ya mchepuo wa kiingereza Enaboishu Academy, ujenzi wa Vituo vipya vya Afya Mwandeti na Oloirieni, pamoja na muindombinu ya barabara.
ARUSHA DC
KaziInaendeleaa✍✍✍✍
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.