Kamati ya Usalama Wilaya Arumeru ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe.Emmanuela M. Kaganda pamoja na timu ya Wataalam toka Halmashauri ya Arusha, wametembelea na kukagua majengo ya shule mpya ya Lemayan iliyopo Kata ya Oldonyosambu. Kamati hiyo ya Usalama Wilaya imeridhishwa na usimamizi wa majengo pamoja na thamani halisi ya fedha iliyotumika. Shule mpya ya Lemayan imejengwa kwa mradi wa Sequip na imeenda kutatua changamoto ya wanafunzi kutembelea umbali wa kilometa 15 kila siku.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.