Wajumbe wa Kamati ya Siasa CCM wilaya ya Arumeru wakikagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa maabara shule mpya ya sekondari Olomotu kata ya Mlangarini.
Mradi huo unatekelezwa kwa gharama ya shilingi milioni 47, milioni 17 zikiwa ni nguvu za wananchi huku milioni 30 zikitolewa na halmashauri fedha za Mapato ya ndani.
ujenzi wa Maabara hiyo ni juhudi za serikali ya wamu ya sita ya kusogeza huduma za kijamii karibu na wananchi na kuhakikisha watoto waote wa kitanzania wanapata elimu karibu na maeneo yao kwa kuondoa changamoto ya kutembea umbali mrefu kwenda na kurudi shukeni.
Hata hivyo Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Arumeru, amepongeza utekelezaji wa mradi huo na kuthibitisha namna Ilani ya CCM inavyotekelezwa kwa vitendo kata ya Mlangarini kwa wananchi na serikali kuchangia maendeleo ya nchi yao.
Ziara hiyo ni maalumu kwa ajili ya ufuatiliaji wa utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2020 - 2025.
"Arusha DC ni Yetu, Tushirikiane Kuijenga"
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.