• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

KAMILISHENI UJENZI WA MADARASA 8000 KWA WAKATI – DKT.MSONDE......

Posted on: November 18th, 2022

Angela Msimbira TABORA


Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughukia Elimu Dkt.Charles Msonde amewataka viongozi wa Mkoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhakikisha wanasimamia na kukamilisha ujenzi wa madarasa 8000 ifikapo Disemba 15,2022 ili wanafunzi wote wanaochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2023 wanapata nafasi.


Ametoa kauli hiyo leo Novemba 18, 2022 wakati akikagua utekelezaji wa maelekezo ya Serikali  hususani kwenye miundombinu  ya shule za Sekondari katika Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge na Uyui Mkoani Tabora.


Dkt. Msonde amesema  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ametoa fedha kiasi cha shilingi biilioni 160 kwa ajili ya kuhakikisha madarasa 8000 yanajengwa katika shule za Sekondari kwa lengo la kuhakikisha watoto wote wanaochaguliwa kujiunga na kidato cha Kwanza mwaka 2023 wanapata nafasi ya masomo.


Dkt. Msonde amesema watoto waliomaliza darasa la saba mwaka huu ni matokeo ya sera bila ada iliyoanzishwa mwaka 2016 na ndio wanaotarajiwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2023, hivyo lengo la Serikali ni kuhakikisha madarasa yanajengwa kwa ajili ya kutatua changamoto ya madarasa nchini.


Amesema kutokana na sera hiyo, kumekuwa na ongezeko kubwa la wanafunzi  kujiunga na elimu ya  msingi hali hii imepelekea  changamoto ya miundombinu ya madarasa kwenye shule za Sekondari nchini hivyo Serikali kwa kuliona suala hilo imeweka mkakati wa kuhakikisha miundombinu ya madarasa inajengwa na kukamilika kwa wakati.


“Mwaka 2021 kulikuwa na Changamoto ya madarasa ambapo watoto waliokuwa wanatakiwa kujiunga na kidato cha kwanza walikuwa zaidi ya 970,000, ambapo uwiano wa wanafunzi wanaomaliza shule kuwa wachache ukilinganisha na wale wanaojiunga na kidato cha kwanza “amesema Dkt.Msonde


Ameendelea kufafanua kuwa mwaka 2023 wanaotarajiwa kujiunga na kidato cha kwanza ni milioni 1.1 wakati wanaotoka ni 430,000, kunatofauti ya wanafunzi 600, hivyo  serikali iliamua kutoa kiasi cha shilingi bilioni 160 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 8000 ili kuongeza madarasa kwenye shule za Sekondari


Amesema kwa upande wa tabora Serikali itajenga madarasa 565 lengo likiwa ni kukabiliana na wanafunzi watakaojiunga na Kidato cha kwanza Mwaka 2023


Kuhusu suala la kuondoa tatizo la watoto kutembea umbali mrefu kufuata masomo Dkt.Msonde amesema Serikali imeweka mkakati wa kulitatua hilo kupitia mradi wa kuboresha elimu ya sekondari (Sequip) ambapo unatarajia kujenga shule za sekondari mpya 1026 ndani ya miaka mitano ambapo shule 26 zitajengwa ambapo kila mkoa kutakuwa na shule moja na shule 1000 zitajengwa katika kila kata.


Aidha amesema katika mwaka wa fedha 2022/2023 Serikali  itatoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa shule 184 ambapo kila Halmashauri inapewa shule moja hivyo serikali imedhamiria kumpunguzia mtoto kutembea umbali mrefu kufuata masomo.


CHANZO: TAMISEMI.





Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.