KAMPUNI YA AIRTEL YAKABIDHI VIFAA VYA INTANENT “ROUTER” KWA HALMASHAURI YA ARUSHA
Kampuni ya Airtel Tanzania kupitia programu yake ya 'Shule Smart' leo tarehe 03/09/2024 imekabidhi vifaa vya mtandao wa intenet 'Router' kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha Bwana Seleman Msumi.
Akipokea vifaa hivyo Mkurugenzi Msumi amewashukuru Kamouni ya Airtel Tanzania kwa kuona umuhimu wa kuzifadhili Shule za Sekondari katika Halmashauri hiyo ili kuongeza morali kwa Wanafunzi kujifunza na kusoma masomo ya Komputa kwani Dunia ya sasa imekuwa ya Kidigitali .
Naye David Nyangaka ambaye ni Afisa TEHAMA Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia aliyeambatana na Uongozi wa Airtel amewahimiza walimu watakaopokea vifaa hivyo kuvitumia kwa umakini na kuvitunza ili kuwasaidia wanafunzi waweze kuwa na Maarifa ya Teknolojia ya Komputa.
Kwa upande wa mwakalishi wa Kampuni ya Airtel Harrison amesema kuwa lengo la Kampuni hiyo kutoa vifaa hivyo ni kurahisisha Wanafunzi kujifunza na kufundishia masuala ya Teknolojia ya Komputa kwa walimu na wananfunzi mashuleni.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.