Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe.Queen Sendiga amesema Serikali imetoa jumla ya shilingi Bilioni 139 katika sekta ya Umwagiliaji katika mikoa ya Kanda ya Kaskazini mwaka wa fedha 2024/25
Ameyasema hayo wakati akifungua maonesho ya 31 ya NaneNane Kanda ya Kaskazini, Agosti 05, 2025 katika Viwanja vya Themi Njiro, Arusha ambapo alikuwa mgeni rasmi.
"Sekta ya Umwagiliaji katika Mkoa wa Arusha unatekeleza miradi ya miundombinu ya Umwagiliaji yenye thamani ya Bilioni 85.24, Mkoa wa Kilimanjaro miradi yenye thamani ya bil.39.1 na Mkoa wa Manyara miradi yenye thamani ya Shilingi bil.15.2," alisisitiza Mhe Sendiga
Aidha, Mhe. Sendiga amewataka wakulima kubadilika kwa kufuata ushauri wa wataalamu wa kilimo ili kuweza kujipatia kipato kizuri wanapofanya shughuli za kilimo.
Kwa upande mwingine amewaomba wadau na Taasisi mbalimbali wawafikie wakulima, wavuvi na wafugaji ili watatue changamoto zao ili waongeze tija katika sekta hizo.
Mbali na hayo, Mhe. Sendiga amewakumbusha wananchi wote kuchagua viongozi ambao watasimama bega kwa bega na wakulima .
Sanjari na hilo, amewaomba washiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu kwa amani, utulivu na bila kuruhusu mazingira ya kuwagawa watanzania kiitikadi, kidini au kikabila.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.