Na Elinipa Lupembe.
Wananchi wa kata ya Laroi halmashauri ya Arusha, wamefanya uzinduzi wa Miongozo ya Elimu iliyotolewa na serikali, huku kina mama wa kata ya hiyo, wakiipongeza serikali ya awamu ya sita na kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa miongozo ya elimu itakayomuwezesha mtoto wa kike kwenda shule.
Kina mama hao wametoa pongezi kwa kuwa miongozo hiyo, imeweka wazi ushiriki wa wazazinkatikamkutekelza sera ya elimu pamoja na ulazima wa kila mtoto mwenye umri wa kwenda shule aandikishwe na kuhakikisha amemaliza elimu ya msingi ya kuanzia darasa la kwanza mpaka kidato cha nne.
Wamesema kuwa, watoto wao watapata fursa ya kuendelea na masomo fursa ambayo kina mama hao wanakiri kutokuipata kutokana na mila na desturi za kabila lao la kimaasai, ambapo watoto wa kike walikuwa wakiishia darasa la saba na kuolewa.
Serikali imetoa mwongozo ambao utawabana wazazi kuwapeleka watoto wote shule, miongozo ambayoo utatoa haki hususani kwa watoto wa kike ambao waliikosa fursa hiyo miaka iliyopita na kuweka wazi kuwa kina mama watahamasishana kuhakikisha watoto wao wanasoma shule kama ilivyokuwa kwa watoto wa kiume.
Hosiana John (mama Lucas Julias) amebainisha kuwa, yeye hakupata nafasi ya kusoma, lakini hujisikia fahari sana anapoona mwanamke msomi, zaidi amepata hamasa zaidi kuwa na Rais mwanamke, na kuahidi kupambana kuhakikisha watoto wake wa kike wanasoma katika jamii yao.
"Kina mama tusirudi nyuma, tupambane kufanya kazi watoto wetu wasome, tulime, tuuze nyanya, vitunguu ili mrafi tuwawezeshe watoto wetu wasome, kama wengine, maendeleo ya kijiji chetu yanaletwa na wasomi hivyo wasomi hao wawe ni watoto wetu". Amesisitiza Mama Hosiana.
"Miongozo hii ingekuja kipindi chetu, hata mimi ningesoma, nimeishia darasa la saba na sikuwa mjinga, nilikuwa nashika nafasi nzuri darasani ila sikupata fursa kama hii, nitahakikisha watoto wangu wanasoma bila kubughudhiwa na kufikia ndoto zao, ninatamani kuona familia zenye vijana wasomi, tutashiriki kuhakikisha watoto wetu wanasoma". Ameweka wazi Dorah Dorian.
Naye Afisa Mtendaji wa Kata ya Laroi, Mneji Bugwema amebainisha kuwa, wananchi wa kata ya Laroi wamepokea miongozo hiyo na kuahidi kushiriki katika utekelezaji wake, hususani kwenye eneo la ushiriki wa wananchi katika kuboresha sekta ya elimu sambamba na kuinua kiwango cha taaluma kwa wanafunzi na kufikianlengonla serikali.
"Miongozo ya elimu imeweka wazi taratibu zote za elimu na malengo yake pamoja na majukumu ya kila mdau wa elimu, kuanzia wanafunzi, walimu, wazazi paomja na viongozi wasimamizi wa elimu, kwa kushirikiana kutekeleza miongozo hiyo kilammmoja kwa nafasi yake, tutafikia malengo ya serikali ya kukuza sekta ya elimu nchini".Amefafanua Afisa Mtendaji huyo
Ikumbukwe kuwa serikali imetoa miongozo mitatu ya elimu itawapa fursa wazazi na walimu kushiriki katika malezi na maadili ya watoto, usimamizi wa wazazi kuchangia chakula cha watoto shuleni, ujenzi na utunzaji wa miundombinu ya shule pamoja na namna bora ya uteuzi wa viongozi wasimamizi wa elimu.
ARUSHA DC
KaziInaendele✍✍
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.