Na. Elinipa Lupembe
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa - TAMISEMI, Prof. Riziki Shemdoe, ameridhishwa na maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa vyumba vya madarasa halamsahuri ya Arusha, wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Arusha ya kukagua miradi inayotekelezwa na fedha zilizotolewa na Serikali Kuu kupitia fedha za mkopo wenye riba nafuu zilizotolewa na Benki ya Dunia ikiwa ni fedha za mpango wa Taifa wa mapambano dhidi UVIKO 19.
Katibu mkuu huyo ameonesha kuridhishwa na hali ya maendeleo ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika halmashauri hiyo, hali inayoashiriakukamilisha ujenzi huo kwa muda uliopangwa kwa kwa tarehe 15.12.2021, huku akiwataka watalamu na wasimamizi wa miradi, kuongeza kasi ya ujenzi na kufanyakazi usiku na mchana pale inapobidi.
"Ninaupongeza uongozi wa halmashauri kwa ujumla wake, kwa kujiongeza na kuamua kujenga majengo ya ghorofa kwenye shule zenye ufinyu wa ardhi hasa shule zilizopangiwa vyumba vingi vya madarasa, changamoto ya ardhi Arusha inafahamika, mmefanikiwa kuongeza ofisi kwenye majengo kwa thamani ile ile ya fedha, kutumia karakana za shule kutengeneza samani za madarasa pamoja na kufanyakazi usiku na machana katika maeneo yenye miradi mikubwa, hongereni sana Arusha DC" ameweka wazi Katibu Mkuu Shemdoe.
Aidha amewataka walimu kujiandaa vema kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza mapema Januari, 2022, kwa kuwa lengo la serikali ni kupunguza msongamano wa wanafunzi madasani ili wanafunzi waweze kujifunzia katika mazingira bora na yenye nafasi, ikienda sambamba na kuwakinga na UVIKO 19 wakati wa kufundisha na kujifunza.
"Serikali yenu ya awamu ya sita, inayoongozwa na Rais wetu mama Samia Suluhu Hassan, inatambua na kuthamini kazi kubwa inayofanywa na walimu ya kufundisha wanafunzi wa Taifa hili, pia inatambua changamoto za kimazingira zinazowakabili walimu, ndio maana imeweza kupandisha madaraja walimu wote wanaostahili, na bado inaendelea kuweka mikakati ya kuboresha maslahi ya watumishi kwa kuzingatia bajeti za serikali yetu, niwatie moyo wa kufanyaka kazi kwa bidii, huku mkiweka uzalendo mbele" a
Hata hivyo walimu wote wa shule za sekondari Kiranyi, Mringa na Matevesi ambao walistahili kupandishwa madaraja, wamethibitisha kupandishwa madaraja katika mwaka huu wa fedha 2021/2022 na tayari mishahara yao imebadilika, jambo ambalo linawatia moyo wa kufanya kazi kwa bidii, huku wakiiamini serikali yao ya awamu ya sita inawajali watumishi hasa walimu ambao idadi yao ni kubwa ukilinganisha na idaid ya watumishi wa sekta nyingine.
Naye Mkuu wa shule ya sekondari Kiranyi, Dkt. Ivan Mmari, amesema kuwa ujenzi wa vyumba hivyo vya madarasa utawezesha mazingira bora ya kujifunzia na kufundishia kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza, waliopangiwa kuanza masomo yao rasmi Januari 2021.
"Shule yetu ya sekondari Kiranyi, imepangiwa jumla ya wanafunzi 800 waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza, mwaka ujao wa masomo, unaotegemea kuanza rasmi Januari 2022, tunajenga jumla ya madarasa 13 ya ghorofa 4 kwa shilingi milioni 260, na tunategemea kukamilisha kwa wakati na kwa ubora unaendana na thamani ya fedha, uwepo wa vyumba hivi vya madarasa licha yabkupunguza msongamano darasani, utaongeza ari katika tendo la kujifunza na kufundisha kwa wanafunzi na walimu pia" Amethibitisha Dkt. Mmari
Katibu mkuu huyo amefanikiwa kutembelea jumla ya shule 3 za sekondari Kiranyi, Mringa na Matevesi na kufanikiwa kukagua jumla ya vyumba 23 madarasa huku halmashauri hiyo, inatekeleza ujenzi wa vyumba 100 vya madarasa, kwa shule 96 za sekondari na vyumba 4 vya madarasa ya shule 2 za Msingi shikizi, kwa gharama ya shilingi bilioni 2,fedha za ruzuku kutoka Serikali Kuu, ikiwa ni fedha za Mpango Maendeleo na Ustawi wa Taifa wa Mapambano dhidi ya UVIKO 19 na madarasa hayo yanategemea kukamilika kabla ya tarehe 15.12.2021.
PICHA ZA ZIARA YA KATIBU MKUU OR-TAMISEMI
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.