Katibu Tawala Wilaya ya Arumeru Ndg Joseph Pascal Mabiti, ameongoza kikao cha tathmini ya Mkataba wa Lishe, kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri chenye lengo la kupokea na kupitia utekelezaji wa Tathmini ya Hali ya Lishe kwa kipindi cha robo ya Nne ya mwaka wa fedha 2024/2025.
Akifungua kikao hicho, Mhe. Mabiti amewataka wajumbe wa kikao hicho kufahamu kuwa lishe ndio msingi wa Afya Bora na Maendeleo Kwa Jamii, na kwamba kikao hicho ni muhimu katika uboreshaji wa lishe katika jamii, ili kuondokana na udumavu.
Mabiti amewataka Maafisa Watendaji wa Kata na Vijiji kuyatekeleza yanayoamuliwa katika vikao, na kutumia vikao na mikutano katika maeneo yao kwa kutoa elimu, ikiwa ni pamoja na kuwaalika Maafisa Lishe katika Kata zao, ili jamii ifahamu umuhimu wa lishe bora, hususan siku 1000 za mwanzo za mtoto, na kuondokana na fikra potofu za lishe bora ni chakula cha "mboga saba".
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha , Ndg . Seleman Msumi amewataka Watendaji wa Kata kuhakikisha wanafanya ufuatiliaji wa afua za lishe, ili kujiepusha na kuhakikisha Kila shule inakuwa na bustani ya mboga mboga kwenye Kila shule na pia kutokutia doa hatua nzuri ya hali ya lishe katika Halmashauri ya Wilaya ya Arusha.
Awali, Kaimu Afisa Lishe Wilaya ya Arusha , Ndg Petro Mfinanga, aliwasilisha taarifa ya utekelezaji ya tathmini ya Lishe katika robo ya Nne(April- Junii) ,na pia Idara na Vitengo vingine viliweza kuwasilisha taarifa zao ikiwemo ,Ustawi wa Jamii kwa mwaka wa fedha 2024/2025, ambapo katika taarifa hiyo, amevitaja vituo vya Afya ,Zahanati na Hospital ya Wilaya kuendelea kutoa matibabu ya utapiamlo ya asili (local treatment) kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano.
Kikao hicho cha tathmini ya Mkataba wa lishe, kimehudhuriwa na baadhi ya Wakuu wa Idara na Vitengo vya Halmashauri, Maafisa Watendaji Kata na wadau wengine wa lishe katika Halmashauri ya Wilaya ya Arusha.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.