• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Kidato cha nne Sokon II, kutumia siku za mapumziko kufanya 'practical' za Sayansi

Posted on: July 9th, 2018

Na. Elinipa Lupembe.

Wanafunzi wa kidato cha nne shule ya sekondari Sokon II wamejihakikishia, kufanya mitihani ya vitendo yaani 'practical' ya masomo ya Sayansi wakati wa mitihani yao ya taifa inayotarajiwa kufanyika mwezi Novemba mwaka 2018.

Uhakikia huo umekuja mara baada ya kukamilika kwa mpigo,  ujenzi wa miundombinu wa maabara tatu za masomo ya Fizikia, Kemia na Baiolojia ambazo tayari wanafunzi hao wameanza kuzitumia kwa ari kubwa.

Wakizungumza na mwandishi wetu shuleni hapo, wakiwa kwenye moja ya chumba cha maabara hizo, wakifanya jaribio la kutafuta Kani ya mvutano 'Force of Gravity' katika somo la Fizikia, wanafunzi hao wamekiri kuelewa zaidi mafunzi ya vitendo kuliko yale ya nadharia.

Wamethibitisha kuwa, kabla ya uwepo wa maabara shuleni hapo, walikuwa na hofu kubwa ya namna watakavyofanya mitihani ya taifa hasa kwenye kipengele cha majaribio ya vitendo, na kukiri kuwa hofu hiyo sasa imetoweka na kuwa na uhakika wa kufanya vizuri na kufaulu masomo hayo.

Wanafunzi hao wamekiri kugundua,  utofauti mkubwa uliopo wa kujifunza kwa nadharia na vitendo kuna urahisi wa kuelewa na kukumbuka kuliko kujifunza kwa nadhari peke yake na kuahidi kuwa kwa kipindi hiki kilichobaki,  watazitumia hadi siku za mapunziko ya Jumamosi na vipindi vya michezo kuhakikisha wamemaliza mada zote katika enoe la 'practical'.

"Miezi mitatu iliyobaki inatosha kutujengea uwezo wa kufanya vizuri na kufaulu mitihani yetu ya mwisho, tumepanga kutumia siku za week end zote kufanya practical". Wamesema wanafunzi hao.

Mwanafunzi Sayuni Elemani amesema kuwa,  ingawa maabara zimetengenezwa ikiwa wamebakiza muda mfupi kabla ya kufanya mitihani yao ya kuhitimu kidato cha nne, wanashukuru na kuongeza kuwa,  wanalazimika kujipanga na kuweka juhudi za ziada, katika  kujifunza kwa vitendo ili waweze kufanya vizuri kwenye mitihani hiyo, kwa kuwa ndio zoezi gumu linalowakabili mbele yao kwa sasa.

Naye mwalimu anayewafundisha wanafunzi hao somo la Fizikia, mwalimu Ahmadi Ponda, amekiri kuwa, licha ya kuwa imebaki miezi mitatu ya kufanya mitihani ya taifa lakini watajitahidi kutumia vizuri kipindi hicho kifupi, kuwajengea uwezo wanafunzi hao wa kuweza kufanya mitihani yao ya majaribio ya vitendo kwa ufasaha.

Hata hivyo Mkuu wa shule yaSekondari Sokon II, mwalimu Mwamvita Kilonzo amesema kuwa, maabara hizo ni neema kwa wanafunzi shuleni hapo kwa kuanza kuyapenda masomo ya Sayansi,  kwa kuwa wanafunzi wengibwalikuwa wakiyachukia na kuyaona ni magumu.

"Kwa sasa wanafunzi wafurahia kuwa na maabara na kufundishwa mada kwa kuzifanya wenyewe kwa vitendo na kuthibitisha kwa machonkile walichojifunza"amesema mkuu huyo wa shule.

Ameongeza kuwa awali iliwalazimu kuwapeleka wanafunzi shule za jirani za sekondari Ilboru na Oldada jambo ambalo lilikuwa likiwapotezea muda mwingi huku kukiwa na matokeo hafifu kwa wanafunzi.

"Kuwapeleka wanafunzi kufanya practical shule za jirani, ilikuwa na changamoto ya gharama na muda ambapo tulitumia siku nzima na kulazimika kuvunja vipindi vingine vya siku.

Aidha Mkuu huyo wa shule amesema kuwa,  uwekaji wa miundombinu ya vyumba hivyo vitatu vya maabara, umegharimu kiasi cha shilingi milioni 25, ikiwa ni fedha za serikali kupitia miradi ya lipa kutokana na matokeo 'Pay for Result P4R'.

Matangazo

  • TANGAZO LA KAZI ZA MKATABA HALMASHAURI YA WILAYA YA ARUSHA August 14, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • MKURUGENZI MTENDAJI WA HALASHAURI YA WILAYA YA ARUSHA BW. SELEMAN MSUMI AWASHONEA SARE MADEREVA WA HALMASHAURI HIYO

    October 02, 2025
  • WIZARA YA KILIMO KUPITIA MAMLAKA YA UDHIBITI WA NAFAKA NA MAZAO MCHANGANYIKO (COPRA) YAZINDUA RASMI MSIMU WA UNUNUZI WA ZAO LA PARACHICHI KWA MWAKA 2025/2026

    September 27, 2025
  • MKUU WA WILAYA YA ARUMERU MWINYI AHMED MWINYI AHITIMISHA MAFUNZO YA JESHI LA KUJENGA TAIFA (JKT)

    September 21, 2025
  • MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA ARUSHA AWAASA WANANCHI KUJENGA UTAMADUNI WA USAFI

    September 21, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.