Wazazi na walezi wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha wametakiwa kuendelea kuchangia chakula cha mchana kwa wanafunzi wa shule za Msingi na sekondari, ili kuongeza kiwango cha ufaulu na kukabiliana na tatizo la udumavu.
Haya yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha , Seleman Msumiambaye ni Mwenyekiti wa Kamati lishe ngazi ya Wilaya kilicholenga kujadili mwenendo wa lishe katika wilaya hiyo.
Seleman Msumi amesema lengo la serikali ni kuhakikisha watoto wanapata lishe bora ili kuwajenga kiafya hatua itakayosaidia kuwa na nguvu kazi ya kutosha kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli na miradi mbalimbali ya maendeleo.
Amesema lishe bora kwa watoto pia itasaidia kuwa na viongozi bora kwa baadaye watakaosimamia vyema shughuli mbalimbali za uzalishaji mali pamoja na kuiongoza nchi.
“Kimsingi ni ngumu sana kwa mwanafunzi kukaa shuleni kuanzia asubuhi mpaka jioni na hajala kitu, ukitaka kuthibitisha hili siku moja andaa kikao cha wazazi kuanzia asubuhi mpaka jioni bila kuwapa kitu cha kula halafu waulize wanajisikiaje, baada ya hapo ndio utajua kwanini serikali inasisitiza umuhimu wa wanafunzi kupata chakula shuleni,” amesema Kiumwa.
Amewataka viongozi pamoja na watendaji wote ngazi ya kata na Vijiji kuchukua suala la lishe kama ajenda ya kudumu kwa kuhakikisha wanatoa elimu kwa wananchi kwenye kila mikutano wanayofanya kwenye maeneo yao.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.