KIKAO CHA TATHMINI YA HALI YA LISHE NGAZI YA WILAYA - ARUSHA DC
Katibu Tawala wa Wilaya ya Arumeru, Bw. Joseph Mabiti, amefungua kikao cha tathmini ya hali ya lishe kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, @amir_mkalipa Mhe. Amir Mohammed Mkalipa.
Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha, leo Tarehe 6, Novemba 2024 na kilihudhuriwa na watendaji wa kata 27 na maafisa tarafa 3.
Madhumuni ya kikao hicho yalikuwa ni kutengeneza mikakati madhubuti kwa ajili ya kuboresha hali ya lishe kwa kushirikisha wahudumu wa afya ngazi ya jamii. Mikakati hii inalenga kubaini familia zenye changamoto za lishe, ikiwemo utapiamlo, na kuwaunganisha na vituo vinavyotoa huduma za lishe na elimu.
Kwa kushirikiana na wadau wa afya, kikao hicho kinatarajia kuboresha huduma za lishe na kuhakikisha familia zinazohitaji zinapata msaada unaostahili ili kupambana na changamoto za afya ya lishe Halmashauri ya Wilaya ya Arusha.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.