Kikao kazi cha maandalizi ya maadhimisho ya Siku ya Mwanamke Duniani kimefanyika leo katika ukumbi wa mikutano ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha chini ya uenyekiti wa Mkuu wa Mkoa Mheshimiwa Paul Christian Makonda.
Katika kikao hicho, wajumbe kutoka Taasisi mbalimbali zikiwemo toka Wizara ya Michezo, Wizara ya Nishati, na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, walishiriki kwa lengo la kuweka mikakati thabiti ya kuhakikisha maadhimisho hayo yanafanyika kwa ufanisi mkubwa.
Akizungumza wakati wa kikao hicho, Mheshimiwa Makonda amesisitiza umuhimu wa kushirikiana kwa karibu ili kuhakikisha kuwa maadhimisho ya mwaka huu yanakuwa yenye tija kwa wanawake wa Arusha na Tanzania kwa ujumla.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.