Halmashauri ya Wilaya ya Arusha yazindua zoezi la umezashaji kinga tiba ya minyoo ya tumbo kwa shule zote za msingi kwa watoto wenye umri wa kuanzia miaka 5 mpaka 14.
Akizindua zoezi Hilo Mwenyekiti Halmashauri ya Wilaya ya Arusha Dkt.Ojungu Selekwa ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayo ongozwa na Dr.Samia Suluhu Hassan kwa kufanikisha upatikanaji wa dawa za kinga tiba ya minyoo ya tumbo kwa Wanafunzi.
"Kwanza tunamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.Samia Suluhu Hassan kwa kutenga kiasi kikubwa Cha fedha kwa ajili ya upatikanaji wa dawa hizi,na sisi kama halmashauri ya Arusha tunamwakikishia kuwa zoezi hili litahitimishwa vizuri".Alisema Dr.Ojungu.
Dkt.Ojungu alitoa wito kwa Wazazi wa wanafunzi pamoja na walimu kuahakikisha wanafunzi hao wanakuwa kwenye mazingira ya usafi ikiwemo kusimamia kunawa mikono kabla ya kula na kuosha matunda kabla ya kuyatumia pamoja na kutumia maji safi na salama.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Wilaya Dkt.Petro Mboya amsema kuwa zoezi hilo la umezeshaji Kinga tiba ya minyoo ya tumbo ni salama na halina madhara yoyote kwa watoto na kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha inazuia na kutokomeza magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele (NTDs) ifikapo 2030.
"Pamoja na zoezi hili nitoe rai kwa wazazi na walezi kuhakikisha wanasimamia vizuri maeneo yao hasa katika usalama wa Afya kwa mtoto, mazingira lazima yawe salama ikiwemo kuhakikisha vyakula wanavyokula watoto vinatayalishwa vizuri pamona na matumizi sahihi ya vyoo".Alisema Dr.Mboya.
Naye Mratibu wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele (NTDs) Ndugu Shabani Mkota alisema zoezi hilo kwa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha ambalo Kiwilaya limezinduliwa katika shule ya msingi Enaboishu limelenga kufikia shule 102 zikiwa za Serikali, na shule za msingi 74 binafsi ikiwa jumla ya shule zote 176 na kwamba zoezi hili litachukua siku mbili kuanzia tarehe 27 na kuhitimishwa tarehe 28 mwezi huu wa pili,huku akitoa rai kwa wazazi na walezi kujitokeza kwa wingi kuleta watoto wao ambao hawajaandikishwa kwenye shule za msingi.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.