Na Elinipa Lupembe
Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mhe. John V.K Mongela amezindua mradi wa nyumba ya mwalimu shule ya msingi Olemedeye iliyopo kijiji cha Kisima cha Mungu kata ya Laroi.
Mkuu huyo wa mkoa amezindua mradi huo ikiwa ni Maadhimisho ya wiki ya Miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, halmashauri ya Arusha.
Mhe. Mongela amewataka wananchi na watanzania kwa ujumla kutambua na kuthamini kazi kubwa iliyofanywa na wasisi wetu Mwl. Julias Kambarage Nyrere na Mzee wetu Sheik Amri Abeid, kazi ambayo matunda yake yanawanufaisha watanzania wote.
Amesema kuwa Muungano huu ni kihistoria duniani kote, nchi mbili kuungana kwa miaka 59 bila kuvunjika ni tunu ya kujivunia watanzania wote, asikubalike mtu yoyote anayediriki kuyumbisha maamuzi ya waasisi wa nch8 hii.
"Tunafahamu Muungano haukutokea hewani, uliundwa na udugu, mwingiliano na uhusiano wa muda mrefu kwa pande zote mbili, waasisi wetu waliweka misingi ya Muungano kwa kuzingatia zaidi kuimiraisha uhusiano wa kijamii, kitamaduni, kiuchumi na kisiasa, misingi ambayo ndiyo inadumu mioyoni mwa watanzania mpaka sasa, tuna wajibu wa kuulinda na kuuenzi Muungano" Ameweka wazi Mkuu huyo wa mkoa
Awali, Mradi huo wa nyumba ya mwalimu, umetekelezwa kwa gharama ya shilingi milioni 50 zikiwa ni fedha kutoka serikali kuu, kwa lengo la kuboresha makazi ya walimu shuleni na kupandisha kiwango cha taaluma shuleni.
KAULIMBIU YA MUUNGANO 2023: "Umoja na mshikamano ndio nguzo ya kukuza uchumi wetu"
ARUSHA DC ni Yetu, Tushirikiane Kuijenga"
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.