LEOPARD TOURS WAKABIDHI PIKIPIKI 20 KWA JESHI LA POLISI ARUSHA.
Kampuni ya Utalii ya Leopard Tours leo tarehe 24/01/2025 imekabidhi pikipiki 20 kwa Jeshi la Polisi Mkoani Arusha ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za kuimarisha ulinzi na usalama Mkoani humo.
Akizungumza wakati akikabidhi pikipiki hizo kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mkurugenzi Mtendaji wa Leopard Tours, bwana Zuher Fazal amesema kuwa hatua hiyo ya kutoa pikipiki kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha imetokana na juhudi zilizofanywa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye Sekta ya utalii ambayo kupitia Royal Tour mapato ya Utalii yameongezeka na hali ya usalama kwa Watalii iko vizuri.
Pia amemshukuru Mkuu wa Mkoa,Mhe Paul Christian Makonda ambaye amekuwa nguzo kubwa kwa kuendeleza juhudi hizo kwenye Sekta ya Utalii kwa kuzingatia kuwa Arusha ndio Kitovu cha Utalii Nchini na kuwa Jeshi la Polisi limekuwa likifanyakazi kubwa ya kuimarisha usalama wa raia na Watalii.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda ameishukuru Kampuni ya Leopard Tours kwa moyo wa kizalendo kujitoa kuisaidia jamii ya wana Arusha na zaidi katika kutoa ajira kwa vijana wa Kitanania katika sekta ya utalii na kinachopatikana katika mapato kukirejesha kwa jamii.
“Moja ya kazi yangu ya msingi katika Mkoa huu ni pamoja na kuweka mazingira mazuri kwa kila mwananchi wa Mkoa huu kutekeleza majukumu yake pasipo bughudha yoyote ile”. Amesema Mhe. Makonda.
Hata hivyo,Mhe.Makonda amelitaka Jeshi la Polisi kuongeza kasi ya kuimarisha Ulinzi na Usalama ili kuhakikisha kuwa Mkoa wa Arusha unakuwa kitovu cha Amani Nchini.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.