Na Elinipa Lupembe.
Wilaya ya Arumeru imeadhimisha siku ya Kumbukumu ya Mashujaa eneo la Usa River halmashari ya Meru ikijumuisha halmashauri mbili za wilaya hizo za Arusha ma Meru
Maadhimisho ambayo hufanyika Julai 25 ya kila Mwaka,Tanzania huadhimisha siku ya kuwakumbuka Mashujaa waliopoteza Maisha yao wakiutetea,Kuupigania na Kulinda Uhuru wa Tanzania. Siku hii pia
Katika wilaya ya Arumeru Mkuu wa wilaya hiyo Mhe. Emmanuela Mtatifikolo Kaganda, amewaongoza wakzi wa wilaya hiyi kuafanya shughuli za kijamii ikiwemo kuomba dua na sala maalumu za kuwaombea Mashujaa waliopoteza maisha pamoja na na kuiombea Amani ya Nchi kutoka kwa Viongozi wa Dini.
Aidha wamefanya zoezi la kuotesha miti 100, kwenye kingo za mto Ndurumanaga, huku vijana wa jeshi la akiba wakiotesha miti mingine 500 kwenye shule mbili, kufanya usafi kuanzia Ofisi za Mkuu wa wilaya, ofisi za makao makuu ya halmashai ya Meru, eneo la Leganga na Kituo cha afya Usa River.
Aidha Mkuu huyo wa wilaya aliongoza maandamano ya amani kutoa ofisini kwake kueleke kituo cha Afya Usa River na kuhitimisha kwa kuwahutubia wananchi.
Kumbukumbu hiyo ya Mashujaa hufanyika ili kuwakumbuka na wakuwaenzi kwa kazi kubwa waliyoifanya ya kulipambania Taifa lao kwa hali na mali kwa ajili ya kuitetea Nchi ya Tanzania wakiwa katika Maeneo mbalimbali.
Mashujaa hao walijizatiti na kujitoa kwa uzalendo wa hali ya juu bila kujali maslahi yao binafsi kwa kujitoa muhannga na kuweka maisha yao rehani na wengine kupoteza maisha kwa ajili ya Tanzania.
Aidha watanzania wote wanatakiwa kuienzi misingi imara ya kizalendo amani na upendo iliyojengwa na waasisi wa Taifa Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere na Sheikh Abeid Amani Karume, misingi ambayo matunda yake tunayafaidi watanzania wote na tujipange kurithisha na vizazi vijavyo.
Katika maadhimishi hayo, Mkuu wa wilaya ya Arumeru, akiwa na Kamati yake ya Ulinzi na Usalama, viongozi wa dini, viongozi wa Chama na Serikali, viongozi wawakilishi wa wananchi pamoja na Watumishi wa halmashari zote mbili za Arusha na Meru.
*MASHUJAA WETU, AMANI YETU!*
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.