• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

MAADIWANI WAIOMBA SERIKALI KUAJIRI WATALAMU WA AFYA NA WATENDAJI WA VIJIJI ARUSHA DC

Posted on: February 10th, 2022

Na Elinipa Lupembe.

Watalamu halmashauri ya Arusha, wameagizwa kuendelea kuikumbusha Serikali, kupata vibali vya kuajiri watumishi, kutokana na upungufu wa watumishi katika sekta ya elimu, afya na utawala, upungufu ambao unakwamisha upatikanaji wa huduma stahiki kwa wananchi.

Rai hiyo imetolewa na wajumbe wa Baraza la waheshimiwa madiwani, kwenye mkutano wa baraza la Madiwani la kuwasilisha taarifa za utekelezaji wa shughuli za kata kwa kipindi cha kuanzia mwezi Oktoba mpaka Desemba 2021, mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo.

Licha ya wajumbe hao, kuwasilisha mafanikio, maendeleo na mipango ya kata zao, waliweka wazi changamoto ya upungufu wa watumishi katika  maeneo yao, changamoto inayokwamisha upatikanaji wa baadhi ya huduma kwa wananchi, ikiwemo maafisa watendaji wa vijiji,  watumishi wa afya katika zahanati na vituo vya afya, pamoja na walimu hasa kata za pembezoni.

Wajumbe hao wameongeza kuwa, serikali kwa kushirikiana na wananchi wamejitahidi sana kuchangia ujenzi wa miundo mbindu ya zahanati, ofisi za vijiji pamoja na vyumba vya madarasa, changamoto inayojitokeza sasa ni upungufu wa watumishi wa kutoa huduma kupitia majengo yaliyojengwa kwa gharama kubwa.

"Tumejenga zahanati, nyingine zimefunguliwa na nyingine yapo majengo tu, lakini hakuna daktari wala wauguzi, ofisi nyingi za vijiji hazina watendaji wa vijiji, tunawaomba watalamu wetu, endeleeni kuisumbua serikali yetu makini, kuajiri watalamu katika maeneo hayo, ili wananchi wetu wapate huduma, kukosekana kwa watalamu kunawavunja moyo wananchi wanaojitolea kujenga miundo mbinu ya kupatia huduma katika maeneo yao" wamesisitiza wajumbe hao.

Aidha Waheshimiwa Madiwani wa kata za Nduruma, Bangata, Oldonyowas, Kiosongo na Musa wamelalamikia ukosefu wa watumishi wa afya kwenye zahanati ambazo tayari zimekamilika ujenzi katika maeneo yao.

Naye Makamu Mwenyekiti wa halmashauri ya Arusha, Mheshimiwa Feddy Mollel, amehitimisha mkutano huo kwa kumuagiza mkurugenzi mtendaji wa  halmashauri hiyo, kuendelea kuwasilisha idadi ya upungufu wa watumishi katika sekta ya afya, idadi ya maafisa watendaji wa vijiji ili serikali iweze kutoa kibali cha kuajiri watumishi hao na kusisitiza kuzisajili zahanati zote ambazo zimekamilika lakini bado hazijapata kusajiliwa.

"Inasikitisha sana, wananchi kwa sasa wana mwamko wa kujiletea maendeleo yao wenyewe, wamejitahidi kujenga miundo mbinu ya zahanati, na kukamilisha, lakini baadhi ya zahanati hazifanyi kazi, kutokana na kukosa watalamu, hii inawakatisha tamaa wananchi wetu, tuiombe serikali yetu sikivu ifanye jambo" amesisitiza Makamu Mwenyekiti huyo.

Akijibu maswali yaliyoulizwa na waheshimiwa madiwani, kuhusu ukosefu wa watumishi katika zahanati na ofisi za vijiji, Afisa Rasilimali watu Halmashauri ya Arusha, Elizabeth Ngobei, amefafanua kuwa,  halmashauri tayari imeomba kibali cha kuajiri Maafisa Watendaji 11 wa vijiji,  huku idadi ya upungufu wa watumishi katika sekta ya Afya, ikiwa imewasilishwa Ofisi ya Rais TAMISEMI, kinachosubiriwa ni kibali cha ajira kutoka serikali Kuu.

Aidha Afisa Rasilimali watu huyo, ameweka wazi kuwa,  licha ya changamoto ya upungufu wa watumishi katika maeneo hayo, serikali inatoa miongozo ya kuwatumia watumishi waliopo, kuhakikisha wananchi wanapata huduma katika maneo yasiyo na watumishi.

"Tunatambua upungufu wa watumishi kisekta,  tumeomba kibali cha kuajiri Maafisa Watedaji 11 wa vijiji, tunasubiri kibali cha ajira kutoka Serikali Kuu, lakini Serikali inatoa miongozo ya kuwatumia watumishi waliopo ili kazi zisikwame na wananchi waendelee kupata huduma licha ya changamoto zilizopo" amesema  Elizabeth 

Hata hivyo Kaimu Mkurugenzi halmashauri ya Arusha, Paulus Kessy, amekiri kupokea maelekezo hayo na kuahidi kuendelea kufuatilia upatikanaji wa vibali vya ajira kwa watumsihi hasa katika zahanati na ofisi za vijiji, maeneo ambayo yanaonekana kupwaya katika upatinaji huduma kwa wananchi, licha ya kuwa suala la upufungufu wa watumishi si la halmashauri ya Arusha pekee bali ni changamoto ya nchi nzima.

Awali katika mkutano huo wa Baraza la Madiwani wa kuwasilisha taarifa za kata, kwa kipindi cha robo ya pili kwa mwaka wa fedha 2021/22, waheshimwa madiwani wa kata zote 27, wameipongeza na kuwa na imani kubwa na Serikali yao ya awamu ya sita, kwa kupelekea fedha nyingi za  miradi ya maendeleo katika maeneo yao, na kuiomba serikali kuendelea kutatua changamoto ndogo ndogo zinazojitokeza katika maeneo yao.


ARUSHA DC

KaziInaendelea✍✍






Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.