Maafisa Maendeleo ya Jamii Jiji la Arusha na Halmashauri ya Arusha, wametakiwa kuvijengea uwezo, vikundi vya wanufaika wa mpango wa kunusuru kaya masikini, kupitia mradi wa mfuko wa Hifadhi ya Jamii - TASAF awamu ya III.
Wito huo umetolewa na Afisa Utumishi na Utawala mkoa wa Arusha, kwa niaba ya Katibu Tawala mkoa wa Arusha, David Lyamongi,
Wakati akifungua mafunzo ya siku tano, kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii ngazi ya kata, yanayofanyika kwenye ukumbi wa mikutano, halmashauri ya Arusha.
Lyamongi, amewataka Maafisa hao, kuhakikisha wanatumia maarifa hayo, kuvijengea uwezo vikundi vya walengwa wa mradi wa kunusuru kaya masikini, katika maeneo yao, ili weweze kuweka na kuwekeza, kwa lengo la kujipatia mitaji na fedha za matumizi wakati wa dharura.
Ameongeza kuwa, lengo la Serikali ni kuwakwamua, wanufaika wa mpango wa kunusu kaya masikini, kutoka kwenye umasikini uliokithiri na kuweza kujikimu kimasha huku, wakijipatia mitaji ya kujiajiri, kuelekea uchumi wa kati.
"Kupitia vikundi vya kuweka na kuwekeza, kaya masikini zitaweza kujikwamua kiuchumi, na kujimudu kimaisha pamoja na kujiajiri, lengo likiwa kupunguza umaskini kuelekea uchumi wa kati" amesema Lyamongi
Naye Mkurugenzi Mtendaji, halmashauri ya Arusha, Dkt. Wilson Mahera, amesema kuwa, endapo vikundi hivyo vitajengewa uwezo na kuweza kujisimamia, halmashauri itawapa mikopo inayotokana na mapato ya ndani ili waweze kujiimarisha zaidi kiuchumi.
Kaimu Mkurugenzi wa Kuendeleza Miradi TASAF Makao Makuu, Abdulmarik Shaban, amefafanua kuwa, baada ya mafunzo hayo, wanategemea kuimarisha uchumi wa kaya masikini, kupitia vikundi vya kuweka na kuwekeza kwa lengo la kuzalishia fedha hizo na kuinua kipato cha kaya masikini.
Shabani, ameongeza kuwa, mradi huu utakapokamilika, kaya masikini, ziwe na uwezo wa kujiendeleza kiuchumi, kwa kufanya shughuli za uzalishaji, ziyakazowawezesha kujikwamua, kutoka kwenye lindi la umasikini, kuelekea uchumi wa kati ifikapo 2025.
Aidha Shabani ameeleza kuwa, wanavikundi hao, wanawekeza fedha hizo, kutokana na fedha wanazopata kupitia mpango wa kunusuru kaya masikini, na kuzitumia kiasi na kiasi kujiwekea akiba kwa ajili ya vipindi vigumu na vya dharura.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.