• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Maafisa Uandikishaji Daftari la Kudumu la Wapiga kura ngazi ya kata, Jimbo la Arumeru Magharibi Wafundwa.

Posted on: July 11th, 2019

Na. Elinpa Lupembe.

Kuelekea kuanza zoezi la kuboresha Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, linalofanywa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi, halmashauri ya Arusha kupitia, Jimbo la Uchaguzi la Arumeru Magharibi, wameanza rasmi mchakato wa uboreshaji wa Daftari hilo, kwa kutoa Mafunzo kwa Maafisa Waandikishaji ngazi ya Kata.

Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo, Mkurugenzi Mtendaji, halmashauri ya Arusha na Afisa Mwandikishaji Mkuu Jimbo la Arumeru Magharibi, Dkt. Wilson Mahera, amewataka, Maafisa Waandikishaji hao, ngazi ya kata, kufuatilia kwa umakini mafunzo hayo, yanayotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ili kuweza kusimamia zoezi hilo kwa uadilifu ndani ya kata zao.

Dkt. Mahera, amewasisitiza kuwa, kazi hiyo ni nyeti na inahitaji umakini na uadilifu wa hali ya juu,  ili kutimiza lengo la Serikali la kuandikisha na kuboresha taarifa za wananchi kwa ajili ya maandalizi ya Uchaguzi mkuu, unaotegemea kufanyika mwaka ujao 2020.

Amewataja watu wanaotakiwa kujiandikisha ni wananchi wote ambao wamefikisha miaka 18 sasa na wale wanaotegemea kutimiza miaka 18, ifikapo tarehe 28.10.2020, pamoja na kuboresha taarifa za watu ambao wamehama kutoka eneo waliloandikisha mwaka 2015 na kuhamia eneo jingine, watu ambao wamepoteza vitambulisho vyao vya kupigia kura.

Naye Afisa Uchaguzi, Halmashauri ya Arusha, Hadija Mkumbwa, amefafanua kuwa, zoezi hilo linategemea kufanyika kwa muda wa siku 7 tu, kuanzia tarehe 18 -24 Julai, 2019, na kufanyika katika vitongoji vyote vya  kata 27, za Jimbo la Arumeru Magharibi, kukiwa na jumla ya vituo 255 vya kujiandikishia.

Hata hivyo mafunzo hayo, yaliambatana na Kiapo cha Kutunza Siri, kilichofanya na Maafisa Waandikishaji ngazi ya kata mbele ya Hakimu Mkazi Mahakama ya Wilaya ya Arusha, Patricia Kisinda.

Hakimu Kisinda, amewapisha Maafisa Waandikishaji hao ngazi ya kata kwa mujibu wa kanuni ya 7(a) ya uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura kwa uchaguzi wa Rais na Wabunge na Kanuni ya 19(a) ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la wapiga kura, Uchaguzi wa Madiwani za mwaka 2018.


Maafisa Uandikishaji ngazi ya Kata Jimbo la Arumeru Magharibi, wakila kiapo cha kutunza siri na kufanyakazi ya Uandikishaji Daftari la Kudumu la Wapiga Kura  kwa uadilifu.

Maafisa TEHAMA wakiandaa mashine ya BVR Kit , tayari kwa kutoa mafunzo kwa vitendo kwa Maafisa Uandikishaji ngazi ya Kata, Jimbo la Arumeru Magharibi.


Hakimu Mkazi Patricia Kisinda, Mahaka ya Hakimu Mkazi Arusha akiwaapisha Maafisa Uandikishaji ngazi ya Kata, Jimbo la Arumeru Magharibi kwenye Ukumbi wa Mikutano, Halmashauri ya Arusha.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.