Na Elinipa Lupembe
Maafisa Watendaji wa vijiji vitatu vya kata ya Laroi, wakisaini mkataba wa Lishe, tayari kwa kwenda kuutekeleza kwenye vijiji vyao.
Maafisa watendaji hao wamesainishwa mkataba huo na Afisa Mtendaji wa kata ya Laroi , Mneji Bugwema na kuwataka kwenda kuutekeleza kwenye vijiji vyao kwa kuzingatia vigezo tisa vya kitaifa vilivyoelekezwa
Bugwema amefafanua kuwa, mkataba huo una lengo la kufanikisha suala la kuboresha hali ya lishe na kupunguza athari za utapiamlo kwa kuhakikisha jamii inashiriki ipasavyo kupanga, kutekeleza na kufuatilia maendeleo ya utekelezaji wa mpango wa halmashauri wa afua za lishe.
Maafisa watendaji wa vijiji hivyo vitatu wamekiri kupokea maelekezo yote yaliyoainishwa na wanakwenda kuufanyia kazi kwa kuzingatia vigezo vilivyoainishwa kwa kushirikiana na maafisa afya ngazi ya jamii katika maeneo yao.
Aidha mkataba wa lishe unawataka Maafisa Watendaji wa Kata kuhakikisha wanashirikiana na Maafisa Watendaji vijiji, kufanya kazi hiyo pamoja na kufanya tathmini na kutoa ripoti ya utekelezaji kwa kila mwezi.
"Lishe duni inasababisha umasikini katika Taifa kwani hakutakuwa na Jamii inayoweza kujituma kwa kufanya kazi kutokana na watu wengi kuathiriwa na utapiamlo, viongozi wenzangu tupambane kutokomeza utapiamlo katika maeneo yetu".
ARUSHA DC
KaziIendelee✍
PICHA ZA WATEDNAJI WAKISAINI MKATABA WA LISHE
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.