Maafisa Watendaji wa Vijiji 34 halmashauri ya Arusha, wakifuatilia mafunzo ya mfumo wa malipo ya Serikali 'Financial Accounting and Reporting System' (FFARS)
Naye mratibu na mwezeshaji wa Mafunzo ya Mfumo huo wa FFARS halmashauri ya Arusha, Joseph Chenya, amesema kuwa mafunzo hayo ni muhimu kwa watumishi wote wa Umma, wanaohusika na mifumo ya mapato na matumizi ya fedha za serikali, ili kuwapa furasa kupata uelewa wa pamoja wa kuufahamu vizuri mfumo, pamoja na matumizi sahihi ya mfumo huo na fedha za Umma.
"Mfumo huu pia utawezesha matumizi ya fedha kulingana na bajeti iliyopitishwa, upatikanaji rahisi wa taarifa mbalimbali kutoka kwenye vituo vya kutolea huduma ikiwemo taarifa za mapato ya kila mwezi, hivyo mkiutumia vizuri mfumo huu, utawarahisishia kazi na kutuondelea hoja za ukaguzi zisizo za lazima" Amesema Chenya
Ameongeza kuwa FFARS imeunganishwa na mifumo mingine ya Serikali ikiwemo mfumo wa PlanRep unaoandaa na kutoa taarifa za utekelezaji wa bajeti pamoja na kuonesha mapokezi ya fedha na fedha zilizoingia kwenye akaunti za vituo na vijiji husika.
Aidha Mratibu huyo amefafanua kuwa, halmashauri ina jumla ya vijiji 67 hivyo watendaji wa vijiji watapewa mafunzo kwa makundi mawili ili waweze kufikiwa wote na kuoata uelewa wa pamoja kwa kuufahamu mfumo vizuri na matumizi sahihi ya mfumo huo.
ARUSHA DC NI YETU, TUSHIRIKIANE KUIJENGA
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.