Na. Elinipa Lupembe.
Karibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Prof. Riziki Shemdoe, amewaagiza wakurugenzi wa halmashauri zote nchini, kufanya uhakiki wa madeni ya waastafu wote, ambao hawajakamilishiwa malipo ya mafao yao, na kuyawakilisha ofisini kwake, ili serikali iweze kufanya utaratibu wa kuwalipa wastaafu hao.
Katibu Mkuu huyo ameyasema hayo, wakati akizungumza na walimu wa shule tatu za sekondari halmashauri ya Arusha, akiwa kwenye ziara ya kikazi, ya kukagua maendeleo ya ujenzi vyumba 100 vya madarasa, mradi unaotekelezwa kupitia fedha maalum za mapambano dhidi ya UVIKO 19.
Prof. Shemdoe amefafanua kuwa, amepokea malalamiko kutoka kwa baadhi ya wastaafu kuwa, kuna baadhi yao hwajalipwa mafao yao huku baadhi hawajakamilishiwa baadhi ya stahiki zao, ikiwemo fedha za kusafirisha mizigo, baadhi ya mapunjo ya mishahara yao.
"Ninawaagiza wakurugenzi wote nchini, kufanya uhakiki kwa wastaafu katika halmashauri zenu, na kubaini wale ambao hawajakamilishiwa malipo yao, ili tujipange namna bora ya kukamilisha malipo yao, serikali inatambua kazi kubwa iliyofanywa na wastaafu hao, kwa kuitumikia nchi katika kipindi chote cha utumishi wao wa Umma, hivyo hatuna budi kahakikisha wanalipwa stahiki zao kwa kuwa ni haki yao" amesisitiza Katibu Mkuu huyo.
Katika ziara hiyo Katibu mkuu huyo, ametembelea shule za sekondari Kiranyi, Mringa na Matevesi na kukagua maendeleo ya ujenzi wa vyumba 26 vya madarasa licha ya kuridhishwa na hatua zilizofikiwa, amewataka wasimamizi na watekelzaji wa mradi huo kuongeza kasi kwa kufanya kazi usiku na mchana ili kukamilisha kwa muda uliopangwa na serikali.
ARUSHA DC
#KaziInaendela✍✍
PICHA ZA MATUKIO YA ZIARA
Katibu Mkuu OR -TAMISEMI Prof. Riziki Shemdoe akitoa maelekezo kwa mkurugenzi Mtendaji, halmashauri ya Arusha, Selemani Msumi ( wa kwanza kulia) mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la ghorofa 4 lenye vyumba 13 vya madarasa shule ya sekondari Kiranyi, mradi unaotekelezwa kupitia fedha za Mapambano dhidi ya UVIKO 19
Katibu Mkuu OR -TAMISEMI Prof. Riziki Shemdoe akizungumza na walimu wa shuke ya sekondari Kiranyi, mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la ghorofa 4 lenye vyumba 13 vya madarasa shuleni hapo, mradi unaotekelezwa kupitia fedha za Mapambano dhidi ya UVIKO 19
Katibu Mkuu OR -TAMISEMI Prof. Riziki Shemdoe akizungumza na walimu wa shuke ya sekondari Mringa, mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa vyumba 10 vya madarasa shuleni hapo, mradi unaotekelezwa kupitia fedha za Mapambano dhidi ya UVIKO 19
Katibu Mkuu OR -TAMISEMI Prof. Riziki Shemdoe katika picha ya pamoja na walimu wa shuke ya sekondari Kiranyi, mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la ghorofa 4 lenye vyumba 13 vya madarasa shuleni hapo, mradi unaotekelezwa kupitia fedha za Mapambano dhidi ya UVIKO 19
Katibu Mkuu OR -TAMISEMI Prof. Riziki Shemdoe katika picha ya pamoja na walimu wa shuke ya sekondari Matevesi,, mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa vyumba 3 vya madarasa shuleni hapo, mradi unaotekelezwa kupitia fedha za Mapambano dhidi ya UVIKO 19.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.