Na Elinipa Lupembe
Madiwani halmashauri ya Arusha, wamemshukuru mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mama Samia Suluhu Hassani na serikali ya awamu ya sita kwa miradi mikubwa, inayotekelezwa na serikali katika halmashauri hiyo.
Shukrani hizo zimetolewa na wajumbe wa kamati ya Fedha, Utawala na Mipango, wakati wa kikao cha majumuisho, mara baada ya ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa kipindi cha robo ya nne na ya mwisho kwa mwaka wa fedha 2021/2022, kikao kilichofanyiaka kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo.
Madiwani hao wameweka wazi kuwa, serikali ya awamu ya sita, imetekeleza miradi mikubwa, ambayo imeanza na kukamilika katika sekta ya elimu, afya, maji, pamoja na uwezeshaji wananchi kiuchumi kupitia asilimia kumi ya mapato ya ndani ya halmashauri.
Mwenyekiti wa halmashauri ya Arusha, Meshimiwa Ojung'u Salekwa, ameweka wazi kuwa miradi iliyotekelezwa katika halmashauri hiyo haijawahi kutokea hapo awali, huku akiwapongeza wananchi na timu ya watalamu kwa usimamizi uliothabiti, unaoifanya miradi kuwa yenye ubora unaoendana na thamani ya pesa iliyotolewa na serikali.
"Tuna kila sababu ya kumshukuru na kumpongeza mheshimiwa Rais, mama Samia, kupitia miradi mikubwa iliyotekelezwa ndani ya halmashauri yetu, miradi ambayo ina tija kwa wanachi wetu, hakika Ilani ya Chama cha Mapinduzi imetekelzwa kwa vitendo" amesisitiza Mwenyekiti huyo
"Tunaipongeza serikali kwa kutoa fedha za kutekeleza miradi ya elimu na afya, matokeo ya miradi hii, inaleta tija kwa wanachi wa kata zetu na Taifa, ninaipongeza timu ya watalamu ikiongozwa na mkurugenzi, kamati za ujenzi kwa usimamizi imara, uliofanikisha kukamilika kwa miradi yenye viwango vya ubora unaoonekana hata kwa macho" amesema Diwani wa kata ya Oldonyosambu Mhe. Raymond Lairumbe
"Ninaipongeza serikali ya awamu ya sita, kwa kutoa fedha nyingi za miradi, hapa tunaona milioni 470 za SAQUIP, zimejenga shule mpya ya sekondari kata ya Kiutu, kata ambayo haikuwa na shule ya sekondari, lengo likiwa kila mtoto apate elimu ndani ya kata yake sambamba na kupunguza msongamano wa wanafunzi kwenye shule za jirani zilizokuwepo" Amebainisha Diwani wa kata ya Olturoto Mhe. Baraka Simon
"Ninaipongeza serikali kupitia TASAF, licha ya kutoa ruzuku kwa kaya masikini katika kata ya Kiutu, lakini imetoa fedha za kujenga kivuko, kivuko ambacho kimeleta amani na utulivu kwa wananchi ambao walikuwa wanakabiliwa na changamoto ya kuvamiwa na kuporwa mali zao na vibaka na wengine kubakwa katika eneo hilo" Ameema Diwani wa kata ya Moivo Mhe. Selina Mollel.
"Ninaipongeza serikali kwa kutekeleza miradi kupitia foeced akaunti, utaratibu ambao unawapa nafasi wanachi kushiriki hatua zote katika utekelezaji wa miradi, jambo ambalo linaongeza wigo wananchi kuimiliki miradi hiyo na kuona ni mali yao" Amesema Diwani Viti Maalum, Mhe. Aneth Kifwe.
Wajumbe wa kamati ya Fedha, wametembelea na kukagua miradi, yenye thamani ya shilingi milioni 607, ikiwemo ujenzi wa shule mpya ya Kiutu milioni 470, milioni 60 ujenzi wa madarasa 3 sekondari Sokon II, milioni 67.1 ujenzi wa kivuko Moivo, kikundi cha Vijana kilichopewa mkopo wa shilingi milioni 10 ikiwa ni asilimia 4 za mapato ya ndani ya halmashauri.
ARUSHA DC
#KaziInaendelea
JIANDAE KUHESABIWA
PICHA ZA MATUKIO WAKATI WA MAADHIMISHO YA KUMBUKUMBU YA SIKU YA MASHUJAA 2022
Wajumbe wa kamati ya Fedha, Utawala na Mipango wakikagua mradi wa ujenzi wa shule mpya ya sekondari Kiutu, mradi unaotekelezwa kwa gharama ya shilingi milioni 470 fedha za miradi ya SEQUIP
Wajumbe wa kamati ya Fedha, Utawala na Mipango wakikagua mradi wa ujenzi wa vyumba vya madarasa shule sekondari Sokoni II, mradi unaotekelezwa kwa gharama ya shilingi milioni 60 fedha za mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA)
Wajumbe wa kamati ya Fedha, Utawala na Mipango wakikagua mradi wa ujenzi wa Kivuko, mradi ulliotekelezwa kwa gharama ya shilingi milioni 60 fedha za Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.