• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

MADIWANI ARUSHA DC, WAIDHINISHA BILIONI 57.1 KUTUMIKA MWAKA UJAO WA FEDHA 2021/2022

Posted on: February 25th, 2021

Na. Elinipa Lupembe.

Wajumbe wa Baraza la Madiwani halmashauti ya Arusha, wameidhinisha mpango wa bajeti ya mapato na matumzi kwa mwaka ujao wa fedha wa 2021/2022, wakati wa mkutano maalum wa Baraza la madiwani uliofanyika kwenye ukumi wa mikutano halmashauri ya Arusha.

.Wakizungumza wa wakati wa  mkutano huo maalumu wa Baraza la Madiwani, wajumbe hao wameupongeza mpango huo wa bajeti ambao, kimsingi wamethibiyisha umezingatia vigezo vya uandaaji wa bajeti pamoja na kugusa maeneo yote kisekta, huku kipaumbele kikubwa ikiwa ni uboreshaji sekta ya elimu kwa kuboresha mindombinu na kuwa na mazingira bora ya kufundishia na kujifunzia.

Mwenyekiti wa halmashauri ya Arusha, Mheshimiwa Ojung'u Salekwa, amesema kuwa fedha hizo kiasi cha bilioni 57.1 zimelenga zaidi katika kutatua kero na changamoto mbalimbali za wananchi wa halmashauri ya Arusha, licha ya kwamba bado halmashauri inakabiliwa na tatizo la miundombinu mibovu ya barabara na maji katika maeneo ya pembezoni, pamoja na uhakika wa  wananchi kupata maji na salama kwa zaidi ya asilimia  30.

Naye Diwani a kata ya Moivo,mheshimiwa Selina Mollel, ameupongeza mpango huo wa bajeti kwa kusema kuwa, ni bajeti yenye matumaini makubwa kwa wananchi, kwa kuwa imejikita kutatua changamoto zilezile zinazowakabili wananchi za ubovu wa miundombinu ya bararabara, maji na umeme, hivyo endapo itatekelezwa kwa kuzingatia viapumbe vilivyowekwa, wananchi wataongeza imani na matumaini makubwa kwa serikali yao.

Hata hivyo, mkurugenzi mtendaji, halmashauri ya Arusha, Saad Mtambule ameviainisha vipaumbele vya halmashauri katika mpango huo wa bajeti kwa mwaka ujao wa fedha  ni pamoja na ukamilishaji na uboreshaji wa miundombinu katika sekta ya Elimu na Afya, kuboresha mfumo wa ukusanyaji wa mapato pamoja na kuongeza vyanzo vya mapato.

Ameongeza ili kufikia lengo la ukusanyaji wa mapato ya ndani ya shilingi bilioni 4.2, halmashauri imejipanga kuboresha na kuongeza vyanzo vya mapato ikiwa ni pamoja na  kufanya urasimishaji wa makazi eneo la Kiseriani, kujenga eneo la uwekezaji utakaokutanisha pamoja vikundi vya wajasiriamali  'industrial area', kujenga shule nyingine ya mchepuo wa kiingereza pamoja na kuboresha machinjio ya Ngaramtoni na kuendeleza kitalu cha mchanga Mirongoine.

"Tunatamani mapato yetu yaongezeke kutoka bilioni 4 mpaka kufikia bilioni 6 kwa kuhakikisha tunakusanya ipasavyo, hasa kupitia sekta ya ardhi, ili tuweze kutatua changamoto zinazowakabili wananchi wetu na kuifanya jamii kuwa na maendeleo endlelevu" amesisitiza mkurugenzi Mtambule.

Akiwasilisha rasimu ya mpango wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2021/2022, kwa niaba ya mkurugenzi mtendaji, Afisa Mipango halmashauri ya Arusha , Anna Urio, ameweka wazi kuwa, halmashauri imepanga kukusanya na kutumia kiasi cha shilingi Bilioni 57.1 huku kukiwa na ongezekomla mapato ya ndani la shilingi milioni 203, sawa na onhezekomla asilimia 4.2 kwa mwaka wa fedha unaoendelea wa 2020/2021, bajeti ambayo utekelezaji wake utategemea vyanzo vikuu vinne. 

Afisa Mipango huyo amefafanua kuwa, utekelezaji wa bajeti hiyo ya shilingi bilioni 57.1, unategemea mapato ya ndani kwa shilingi bilioni 4.4, bilioni 1.5 fedha kwa ajili ya matumizi mengineyo, bilioni 10.2 ikiwa ni Ruzuku ya miradi ya maendeleo huku ruzuku ya mishahara ya watumishi ikikadiriwa kutumia kiasi cha shilingi bilooni  40.8  ikiwa ni asilimia 72.54 ya bajeti yote, bajeti ambayo inategemea serikali kuu kwa zaidi ya asilimia 90.

Rasimu hiyo ya mpango wa bajeti ya halmashauri ya Arusha, kwa mwaka wa fedha 2021/2022 licha ya kuidhinishwa na mkuatano wa Baraza hilo la Madiwani, bado inaendelea kuwa rasimu mpaka kukamiliaka kwa michakato yote ya kisheria na hatimaye kufikia kuidhinishwa na Bunge la Jamhuri ya Muunga wa Tanzania ili kuanza utekelezaji wake ifikap Julai 1, 2021.


Afisa Mipango halmashauri ya Arusha, Anna Urio, akiwasilisha rasimu ya mpango wa bajeti ya mapato na matumzi ya halamshauri hiyo, kwa mwaka wa fedha 2021/2022 mbele ya wajumbe wa baraza la madiwani, mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano halmashauri ya Arusha.


Baadhi ya wajumbe wa Baraza la madiwani, wakifuatilia uwasilishwaji wa rasimu ya mpango wa bajeti ya mapato na matumzi ya halmashauri ya Arusha, kwa mwaka wa fedha 2021/2022 kama ilivyokuwa ikiwasilishwa na watalamu wa halamshauri hiyo wakati wa mkutano maalum wabaraza  la madiwani, uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano halmashauri ya Arusha.


Baadhi ya wajumbe wa Baraza la madiwani, wakifuatilia uwasilishwaji wa rasimu ya mpango wa bajeti ya mapato na matumzi ya halmashauri ya Arusha, kwa mwaka wa fedha 2021/2022 kama ilivyokuwa ikiwasilishwa na watalamu wa halamshauri hiyo wakati wa mkutano maalum wabaraza  la madiwani, uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano halmashauri ya Arusha.

Baadhi ya wajumbe wa Baraza la madiwani, wakifuatilia uwasilishwaji wa rasimu ya mpango wa bajeti ya mapato na matumzi ya halmashauri ya Arusha, kwa mwaka wa fedha 2021/2022 kama ilivyokuwa ikiwasilishwa na watalamu wa halamshauri hiyo wakati wa mkutano maalum wabaraza  la madiwani, uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano halmashauri ya Arusha.

Diwani wa kata ya Olturoto, mheshimiwa Baraka Simon, akichangia hoja wakati wa mkutano wa kujadili rasimu ya mpango wa bajeti ya halamshauri ya Arusha kwa mwaka wa fedha 2021/2022.

Diwani wa Viti Maalum, mheshimiwa Happy Tarimo, akichangia hoja wakati wa mkutano wa kujadili rasimu ya mpango wa bajeti ya halamshauri ya Arusha kwa mwaka wa fedha 2021/2022.

Diwani wa kata ya Ilkiding'a mheshimiwa Francis Lukumay akichangia hoja wakati wa mkutano wa kujadili rasimu ya mpango wa bajeti ya halamshauri ya Arusha kwa mwaka wa fedha 2021/2022.

Diwani wa kata ya Kisongo, mheshimiwa Godson Loning'oakichangia hoja wakati wa mkutano wa kujadili rasimu ya mpango wa bajeti ya halamshauri ya Arusha kwa mwaka wa fedha 2021/2022.

Mwakilishi wa meneja wa TARURA halmahauri ya Arusha,  Frank Mwanga, akiwasilisha mpango wa bajeti ya barabara ya kwa mwaka wa fedha 2021/2022.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.