Mafunzo ya siku mbili kwaajili uboreshaji wa Daftari la kudumu la mpiga kura yakiendelea kwa Maafisa Wasaidizi ngazi ya Kata katika Halmashauri ya Wilaya Arusha katika ukumbi wa shule ya Sekondari Ilboru.
Mafunzo hayo ni ya awali kabla kuanza kwa zoezi hilo litakaloanza rasmi tarehe 11-17 /12/ 2024 kwa Mkoa wa Arusha likiwa na lengo la kuwaandikisha wapiga kura wapya, kutoa vitambulisho kwa waliopoteza, kufanya marekebisho kwa kadi zilizoharibika,na kuwaondoa wapiga kura waliopoteza sifa mfano kifo, kupata uraia wa nchi nyingine.
Maafisa Wasaidizi ngazi ya Kata wanaopata mafunzo siku ya leo ya tarehe 04/12/2024 baada ya magunzo hayo,watakuwa na jukumu la kwenda kufundisha Maafisa Waandikishaji wasaidizi ngazi ya Kituo na waendesha vifaa vya BVR.
Aidha zoezi hili la uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura ni kwaajili ya maandalizi ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 kwa nafasi ya Udiwani, Ubunge na nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.