Walengwa wa TASAF walio kwenye mpango wa Kunusuru kaya Masikini kijiji cha Lemong'o kata ya Oldonyosambu, wakipatiwa mafunzo ya uundaji wa vikundi vya kuweka akiba, kuwekeza na kukopeshana.
Mafunzo hayo ni utekelezaji wa programu ya TASAF ya kuwajengea uwezo walengwa hao, kuwa na tabia chanya ya kujiwekea akiba, zaidi kuwekeza fedha za kukopeshana kwa ajili ya kuanzisha miradi ya uzalishaji.
Mratibu wa TASAF Halmashauri ya Arusha Grace Makema, amesema kuwa, vikundi hivyo vitaendelea kusimamiwa na watalamu wa fani za mtambuka za Maendeleo ya Jamii, kilimo, mifugo, biashara na ujasiriamali ili kuviwezesha kubuni miradi midogo midogo ya uzalishaji.
" Uanzishwaji wa vikundi hivyo, unalenga zaidi kuongeza pato la familia kupitia miradi ya uzalishaji watakayokuwa wanaifanya kwa usimamizi wa watalamu kutoka halmashauri". Amefafanua Mratibu Grace
Hata hivyo Mratibu wa huduma za Vikundi TASAF Makao Makuu, Ester Kivuyo, amesema kuwa lengo mafunzo hayo ni kuzijengea uwezo kaya za walengwa kuwa na utamaduni wa kujiwekea akiba na kutumia akiba hizo katika kukopeshana katika vikundi ili kuendeleza miradi ya kiuchumi ili kujiongezea kipato cha kaya.
"ARUSHA DC ni Yetu, Tushirikiane Kuijenga"
#kaziinaendelea✍✍✍✍
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.