MAHAFALI YA JKT OPERESHENI MIAKA 60 YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.
Vijana waliohitimu mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa Oparesheni ya miaka 60 ya Muungano watakiwa kuwa wema ,wenye Utii na kuwa mfano wa kuigwa kwenye Jamii.
Haya yamesemwa na Mkuu wa wilaya ya Arumeru Mhe. Amir Mohamed Mkalipa, wakati akifunga mafunzo ya miezi mitatu ya Oparesheni miaka 60 ya JKT, KJ833 Oljoro, kwa kuwataka vijana hao, kwenda kutumia ujuzi na maarifa waliyoyapata kulitumikia taifa la Tanzanzia pamoja na kuwa mfano wa kuigwa na vijana wenzao ambao hawajapata fursa ya kupitia mafunzo haya ndani ya jamii.
Mhe. Mkalipa licha ya kuwapongeza vijana hao, amewasisitiza kwenda kutekeleza kwa vitendo yale yote waliyojifunza ili kutimiza uahalisi wa mafunzo kwa kuonesha utofauti kati yao na vijana wasioshiriki mafunzo haya kwa kuonesha umahiri na uzalendo kwa nchi yao
"Leo vijana mmeonesha umahiri mkubwa uliotupa taswira ya jinsi wakufunzi wamewafundisha ukakamavu, uzalendo, utiifu na umahiri, mmeitendea haki heshima ya Amiri Jeshi Mkuu, mmeonyesha uaminifu kwake kama JKT na jeshi kwa ujumla, hivyo katumieni maarifa haya kulitumikia Taifa na sio vinginevyo" Amesisitiza Mkuu wa wilaya
Ameongeza kuwa, umefika wakati wa kuanza maisha ya kujitegemea, mmepita kipindi cha uangalizi wa wazazi na walimu, sasa mko tayari kujisimamia, tumieni vizuri uhuru wenu kwa kutekeleza majukumu binafsi na yale mtakayopangiwa kwa kuzingatia kanunia taratibu, sheria za nchi kwa kuheshimu mila na desturi za jamii sambamba na kuepuka tabia hatarishi ikiwemo matumizi yasiyo sahihi ya mitandao, yanaweza kuwaingiza kwenye migogoro ya kisheria.
Hata hivyo wahitimu hao, wameishukuru serikali kwa programu hiyo muhimu kwa vijana wa kitanzania na kukiri kujengewa uwezo mkubwa wa kujitambua na kujithamini, kujiamini na kujitegemea, uzalendo, utiifu, uhodari na umahiri, utakaowawezesha kulitumikia Taifa lao na watanzania kwa ujumla.
Naye Mhitimu 'service' Salvatory Wilson Shange, amesema kuwa mafunzo hayo yamewatoa kwenye ulimwengu wa giza na kuwaleta kwenye mwanga ambao utakuwa dira ya maisha yao katika kulitumikaia Taifa la Tanzania
"Wengi tulikuja tukiwa na hofu kumbwa, kumbe mambo ni tofauti, JKT inatoa mafunzo ambayo yanatujengea uwezo mkubwa wa kuwa vijana wenye kulitumikia Taifa kwa uzalendo na sio ubinafsi" Amesema Salvatory
Mzazi wa John Samwel, ameishukuru Mungu na serikali na kuweka wazi kuwa mwanzo walikuwa na hofu kubwa lakini ameshuhudia mabadiliko makubwa ya kitabia kwa mtoto wake, amezidisha nidhamu, na amekiri kutamani kijana wake kuendelea kubaki jeshini kuliko kubaki mtaani
Awali kwa mamlaka aliyopewa Mkuu wa wilaya ya Arumeru amefunga mafunzo hayo rasmi ambayo ni ya kundi la lazima wamehitimu mafunzo ya oparesheni ya miaka 60 ya Muungano katika kikosi cha JKT Oljoro.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.