Halmashauri ya Arusha imejipanga kutoa mafunzo mafupi kuhusu matumizi sahihi ya fedha za Mpango wa Kunusuru kaya Masikini zinazotolewa na serikali kupitia mradi wa TASAF awamu ya III kwa wanufaika wa Mpango huo kila wakati wa zoezi la malipo ya wanufaika hao linapofanyika.
Uamuzi huo umefikiwa kutokana na baadhi ya waniufaika wa mpango huo kuonekana kutumia fedha hizo kwenye ulevi na mambo mengine yasiyofaa kinyume na malengo ya mradi huo na kusababisha baadhi yao kupunguziwa malipo kutokana na kushindwa kutimiza masharti ya fedha hizo na wengine kusababisha migogoro kwenye familia
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.