Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi, anapenda kuutarifu Umma kuwa Halmashauri imepokea fedha kiasi cha shilingi Milioni 682.5 kutoka Serikali Kuu kupitia Mradi wa Kuboresha Upatikanaji wa Fursa sawa katika Ujifunzaji Bora kwa Elimu ya Awali na Msingi Tanzania Bara (BOOST), fedha zitakazotumika katika ujenzi wa miundombinu ya shule 6 za Awali na Msingi.
Fedha hizo tayari zimeingizwa kwenye akaunti za shule na ujenzi huo utatekelezwa ndani ya miezi mitatu kuanzia sasa, kwa kutumia mwongozo rahisi wa ’Force Account’ uliotolewa mwaka 2023 na kwa kuzingatia taratibu zote za manunuzi na usimamizi wa fedha za Umma.
Aidha utekelezaji wa miradi hiyo utazingatia Ramani na miongozo ya ujenzi iliyotolewa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ya mwaka 2023.
"ARUSHA DC ni Yetu, Tushirikiane Kuijenga"
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.