Na. Elinipa Lupembe
Mkuu wa wilaya ya Arumeru Mhandisi Richard Ruyango ameupokea Mwenge wa Uhuru 2022, katika halmashauri ya Arusha, kwenye viwanja vya shule ya sekondari Oldadai ukitokea halmashauri ya Jiji la Arusha.
Mhandisi Ruyango amekabidhiwa Mwenge huo wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Mheshimiwa Saidi Mtanda, ukiwa unang'ara unameremeta pamoja na wakimbiza Mwenge Kitaifa na Kimkoa, na kuahidi kutunza mpaka siku ya kuukabdhi.
Mkuu wa wilaya huyo ameweka wazi kuwa, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2022, ndugu Sahil Nyanzabara Geraruma atakimbiza Mwenge wa Uhuru takribani Kilomita 90.4, na kupitia jumla ya Miradi 9 yenye thamani ya shilingi Bilioni 4.2 kwenye sekta ya elimu, afya, maji, miundombinu ya barabara na uwekezaji.
Kauli Mbiu ya Mwnge wa Uhuru 202: SENSA NI MSINGI WA MIPANGO YA MAENDELEO
: SHIRIKI KUHESABIWA, TUYAFIKIE MAEMDELEO YA TAIFA"
MWENGE WA UHURU Hoyeeeeeeee
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.