• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

KIVULINI MARTENITY AFRICA MKOMBOZI WA WAJAWAZITO ARUSHA

Posted on: November 9th, 2022

Na Elinipa Lupembe

Kituo cha afya cha Kivulini  Martenity Afrika kimekuwa mkombozi wa wanawake wajawazito kwa kuwa kituo hicho ni kituo maalum cha kutoa huduma za kujifungua kwa kina mama wajawazito na matibabu ya wagonjwa wa fistula, kikifanikisha kupunguza vifo vya wanawake na watoto wakati wa kujifungua.

Kufuatia utoaji huduma hizo, Kivulini kimeongeza kujenga jengo la kupumzikia wajawazito wenye changamoto za uzazi na wale waliokaribia kujifungua kwa ajili ya kuwa na uangalizi wa karibu wa madaktari kwa mjazito, jengo lenye uwezo wa kupumzisha wajawazito 20, lililogharimu shilingi  milioni 90.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa jengo hilo, Mkurugenzi Mkazi Maternity Africa. Michael Hynds, amesema kuwa, lengo la kuongeza jengo hilo ni kupata wodi ua wapumzisha wajawazito waliokaribia kujifungua na wale wenye changamoto ili kuwa karibu na uangalizi wa madaktari.

"Tumefikia hatua hii, kutokana na changamoto iliyokuwa ya kukosa mahali pa kuwapumzisha wajawazito, jambo ambalo awali lilihatarisha maisha ya kina mama na watoto, lakini kuwepo kwa jengo hili, kutaokoa maisha ya mama na mtoto" . Amesisitiza  Hinds.

Hata hivyo mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha, baada ya kuzindua jengo hilo, ameushukuru uongozi wa Kituo cha Maternity Afica kwa huduma bora za uzazi wanazozitoa kwa kina mama wa kitanzania, huduma ambazo zimesaidia kupunguza vifo vya mama na mtoto wakati wa kujifungua katika halmashauri.

Mkurigenzi Msumi ameongeza kuwa, serikali inathamini huduma ya kipekee inayotolewa na kituo cha Kivulini, kituo ambacho kinafanya kazi kubwa yenye baraka za kiMungu zilizopaswa kufanywa na serikali na kuridhishwa namna wagonjwa wanapatiwa huduma bure bila malipo yoyote.

Muuguzi Mkuu, halmashauri ya Arudha Noemi Themi, amesema, kituo hicho kimepunguza msongamano wa wajawazito kwenye vituo vya serikali kwa mkoa wa Arusha na mikoa jirani,  hususani wale wenye changamoto za uzazi na ugonjwa wa fistula.

Nao wagonjwa waliolazwa kwenye kituo hicho cha afya, wameponheza na kushukuru huduma bora inayotolewa hapo bila malipo yoyote ikiwemo, matibabu, malazi ma chakula, jambo ambalo limeokoa maisha ya familia zisizo na uwezo.

 Suzana Msami (26) mkazi wa Muleba mkoani Kagera, amethibitisha kutibiwa ugonjwa wa Vistula, ugonjwa ambao alihangaika nao kwa muda mrefu kwenye hospitali za Muleba na Bugando bila mafanikio

"Nilipataa rufaa kutoka hospitali ya Bugando, na nimetibiwa kwa sasa ninaendelea vizuri, sikuwa na pesa za matibabu, hapa nimetibiwa bure na kupatiwa huduma za chakula na malazi bure, ninamshukuru Mungu ninawashukuru madaktari na wauguzi kwa upendo uliorejesha furaha na matumaini ya maisha yangu tena" .Amesisitiza Suzana

Kituo cha Afya Maternity Africa kilifunguliwa mwaka 2018 na mpaka sasa jumla ya akinamama 8500 wamejifunguliwa kituoni hapo huku zaidi ya wagonjwa 550 wametibiwa ugonjwa wa Fistula na wanategemea sasa kuhudumia zaidi ya wagonjwa elfu tatu kwa mwaka.

ARUSHA DC

KaziInaendelea









Matangazo

  • TANGAZO LA KAZI ZA MKATABA HALMASHAURI YA WILAYA YA ARUSHA August 14, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • KUFUATILIA NA USAMIZI WA HAKI ZA MTOTO KATIKA JAMII NI JAMBO MUHIMU

    August 25, 2025
  • RAIS SAMIA AMUAPISHA AMOS MAKALLA KUWA MKUU WA MKOA WA ARUSHA

    August 26, 2025
  • DKT. JAHANNES LEMBULUNG' LUKUMAY ACHUKUWA FOMU YA UGOMBEA UBUNGE WA CCM JIMBO LA ARUMERU MAGHARIBI

    August 25, 2025
  • KIKAO KAZI CHA WENYEVYITI WA BODI NA WATENDAJI WAKUU WA TAASISI ZA UMMA (CEOs Forum 2025)

    August 24, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.