Na Elinipa Lupembe - ARUSHA.
Mbio za maalumu za Kilomita 10 zilizokwenda kwa jina la The Great Health Run, zilizofanyi katika halmashauri ya Arusha, wilaya ya Arumeru, zimefanikisha dhamira ya uchangiaji Damu Salama, ili kuokoa maisha.
Mbio hizo zilizoambatana na zoezi la uchangiaji damu Salama, na kufanikisha kupata uniti 10 za damu, pamoja na ugawaji wa vifaa vya kupimia uzito kwa watoto kwenye vituo vitano vya afya vya halmashauri hiyo.
Mgeni rasmi katika mbio hizo, Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi, amewapongeza waandaji na washiriki wa mbio hizo na kuwataka wananchi kuona umuhimu wa kujitoa kuchangia damu, kwa kuwa uwepo wa damu ya akiba, husaidia kuokoa maisha ya wagonjwa wa dharura katika hospitali nchini.
Aidha ametoa wito wa wananchi kufanya mazoezi binafsi pamoja na kushiriki mbio zinazoandaliwa na wadau mbalimbali, kwa kuwa licha ya kuimarisha afya ya mwili, mazoezi huzuia magonjwa mengi yasiambukiza kama kisukari, uzito uliokithiri pamoja na shinikizo la damu.
"Inafahanika kuwa siri kubwa ya kufanya mazoezi, ni kuimarisha mwili na kuufanya kuwa 'active', mazoezi yanamfanya mtu kuwa kama kijana, kuna wazee wenye zaidi ya miaka 65, tumekiambia nao na ukiwatizama afya zao utadhani vijana, hii ni kutokana na kufanya mazoezi".Amesisitiza Mkurugenzi Msumi
Aidha Mkurugenzi Msumi, amewashukuru watu wote waliojitoa kuchangia damu na kusistiza jamii umuhimu wa kuchangia damu ni pamoja na kuokoa maisha ya watu hususani wagonjwa wa dharura, hivyo kuwa na tabia ya kuchangia damu kila inapobidi.
Naye Kaimu Mganga Mkuu, halmashauri ya Arusha, Dkt. Japhet Champanda amekiri uwepo wa uhitaji wa Damu katika vituo vya kutolea huduma za afya, unaolazimu kuwa na akiba ya damu katika hospitali, na kutumika pindi wanapotokea wagonjwa wanaohitaji kuongezewa damu.
"Tunauhitaji wa damu usiopungua uniti 100 kwa mwezi na uniti 1,200, kwa mwaka, utaona namna uhitaji wa damu ulivyo mkubwa, damu ambayo hutumika zaidi kwa kina mama wakati wa kujifungua, wagonjwa dharura na majeruhi wa ajali". Amefafanua Dkt. Champanda.
Hata hivyo, Dkt. Champanda ameeleza umuhimu wa kufanya mazoezi ya viungo mara kwa mara, kuwa inapunguza magonjwa yasiyo ya lazima, na kusisistiza pamoja na kuzingatia mazoezi, watu wanatakiwa kuzingatia ulaji wa vyakula vyenye lishe bora.
Awali muandaaji wa mbio hizo na Muuguzi wa Zahanati ya Moivo Kilie Ghubi, amesema kuwa mbio hizo zenye lengo la kuchangia damu kuokoa maisha, zimeambatana
na ugawaji wa vifaa vya kupima uwiano wa uzito, urefu na umri kwa watoto wachanga (stadiomita), vifaa vilivyogawiwa kwenye vituo vitano vya afya, halmashauri ya Arusha.
Ghubi amewashukuru watu wote waliojitokeza kushiriki mbio hizo, sambamba na uchangiaji wa damu salama, na kubainisha kuwa jumla ya watu 756 wameshiriki mbio hizo.
SHIRIKI SENSA YA WATU NA MAKAZI 23.AUGUST 2022
JIANDAE KUHESABIWA✍✍✍
PICHA ZA MATUKIO WAKATI WA MBIO ZA THE GREAT HEALTH FUN
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi (wa pili kushoto) akizungumza wakati wa kuhitimisha Marathon ya The Great Health Run kwenye viwanja vya makao Makuu ya Halmashauri ya Arusha.
Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi,
Muandaaji wa Mbio za The Great Health Run, Kilie Ghubi (Kulia) akimkabidhi keki, Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi, wakati wa kuhitimisha mbio hizo, kwenye viwanja vya makao Makuu ya Halmashauri ya Arusha.
Mwenyekiti Halmashauri ya Arusha, mhe. Ojung'u Salekwa akimlisha keki mtoa huduma kutoka Kivulini Martenity, wakati wa kuhitimisha Marathon ya The Great Health Run kwenye viwanja vya makao Makuu ya Halmashauri ya Arusha.
Wahirikim wa Marathon ya The Great Health Run wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi (wa pili kulia) wakati wa kuhitimisha zoezi hilo kwenye viwanja vya makao Makuu ya Halmashauri ya Arusha.
SHIRIKI SENSA YA WATU NA MAKAZI 23, August 2022
JIANDAE KUHESABIWA ✍✍
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.