Mgeni rasmi wa maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima (Nanenane) mwaka 2025, Mhe. Nurdin Hassan Babu, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, akiwa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri za Wilaya kutoka mikoa ya Kanda ya Kaskazini. Picha hiyo ilipigwa mara baada ya hafla kufikia tamati katika Viwanja vya Themi Njiro, Arusha.
Tukio hili lilidhihirisha mshikamano wa viongozi hao katika kuendeleza sekta ya kilimo na kuchochea maendeleo ya wakulima wa Halmashauri hizo na katika mikoa ya kanda hiyo. Aidha, picha hiyo ni kumbukumbu ya ushirikiano wa pamoja wa viongozi hao katika kuhamasisha matumizi ya teknolojia na mbinu bora za kilimo.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.