Mapema leo, tarehe 08 Agosti 2025, Mhe. Nurdin Hassan Babu, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, akiwa ameambatana na mwenyeji wake, Mhe. Kenani Laban Kihongosi, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, wametembelea Banda la Halmashauri ya Wilaya ya Arusha katika Maonesho ya Wakulima (Nanenane) yanayoadhimishwa kimkoa katika Viwanja vya Nanenane, Themi Njiro, Arusha. Ziara hiyo ilikuwa sehemu ya ratiba ya viongozi hao kutembelea mabanda mbalimbali ili kujionea ubunifu na teknolojia mpya zinazotumika katika sekta ya kilimo.
Katika ziara hiyo, viongozi hao walipokelewa na Maafisa Kilimo, Mifugo na Uvuvi wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha, ambao waliwasilisha maelezo kuhusu huduma na bidhaa zinazotolewa kupitia sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi. Pia walionesha mbinu za kisasa za kilimo cha mazao mbalimbali, ufugaji wa kisasa, na teknolojia za kuongeza thamani ya mazao ili kuongeza kipato cha wakulima.
Mhe. Nurdin Hassan Babu alipongeza juhudi za Halmashauri ya Wilaya ya Arusha katika kuhamasisha wakulima kutumia mbinu za kisasa na kuongeza uzalishaji. Aidha, aliwasisitiza wakulima na wananchi kwa ujumla kushiriki kikamilifu maonesho haya ili kujifunza mbinu mpya na kupata maarifa yatakayowawezesha kuboresha maisha yao kupitia kilimo chenye tija.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.