• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

MHE. RAIS SAMIA AWAAHIDI MAJI WANANCHI WA KISONGO

Posted on: November 28th, 2022

Na Elinipa Lupembe

Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amewaahidi wananchi wa Kisongo kuwasiliana na Wizara ya maji kuona namna ya kuunganisha  mradi wa maji wa bilioni 600 wa Jiji la Arusha ili kuwafikia wananchi hao.

Mhe. Rais ameyasema hayo kwenye Mkutano wa Hadhara, uliofanyika kwenye soko la Kisongo kata ya Mateves, Halmashauri ya Arusha, wilaya ya Arumeru, wakati akiwaaga wananchi wa mkoa wa Arusha mara baada ya kumaliza ziara yake mkoani humo.

"Tumemaliza tatizo la maji Jiji la Arusha kupitia mradi wa maji wa Bilioni 600, mahitaji ya Jiji la Arusha ni lita milioni  90 tu, na maji hayo yamezidi, tutafanya mpango kuhakikisha maji hayo yanaunganishwa hapa, ili wananchi wa Kisongo mpate maji, Kisongo maji yatapatikana". Amesema Mhe. Rais

Mhe. Rais amewahakikishia wana Kisongo maji na kuongeza kuwa Wizra ya maji inatekeleza miradi mingi kwa sasa, ikitokea bakaa yoyote ipelekwe Arumeru ili kumaliza tatizo hilo.

Katika mkutano huo, Mbunge wa Jimbo la Arumeru Magharibi, Mhe. Noah Lembris alipata fursa ya kuwasilisha changamoto zinazowakabili wananchi wa Jimbo hilo ikiwemo miundombinu ya barabara za ndani, maji, ujezni wa soko la Kisongo pamoja na mpaka wa mita 200 kati ya Arusha DC na Jiji la Arusha.

Aidha Mbunge huyo licha ya kuwasilisha changamoto hizo amemshukuru na kumpongeza Mhe. Rais kwa serikali kutoa fedha za utekelezaji wa miradi ya maendeleo jimboni humo.

"Kupitia TARURA tumepokea bilioni 1.5 za ujenzi wa barabara za ndani, umesaini mkataba wa bilioni 22 za ujenzi wa barabara ya lami Km 18 Mianzini, Timbolo- Ngaramtoni, milioni bilioni 1,4 za kukamilisha vituo vya afya, milioni 450 kumaliza zahanati 11 lakini pia tumepokea milioni 760 za ujenzi wa madarasa 38 shule 15 za sekondari kwa ajili ya wanafunzi wankidato cha kwanza 2023". Amebainisha Mhe. Noah.

Hata hivyo Katibu Mkuu TAMISEMI Prof. Riziki Shemdoe ameitaja mikakati ya ujenzi wa barabara za ndani katika halmashauri hiyo na kusema kuwa serikali itazingatia mahitaji yaliyowasilishwa na kuweka kwenye mpango wa bajeti kwa mwaka ujao wa fedha.

"Ujenzi wa soko ni mradi mkakati, nitamuelekeza Mkurugenzi wa halmashauri ya Arusha, kuandika andiko likikidhi vigezo, tutakaa na Wizara ya fedha ili mrafi huu uanze". Amesema Katibu mKuu huyo.

Hata hivyo Mhe. Rais ametumia fursa hiyo kuwaaga wananchi wa Arusha na kuweka wazi kuwa atarudi Arusha kwa kuwa, Arusha ni kiini cha shughuli za za Serikali na mataifa ya nje.

Awali, Mhe.  Rais amefanya mkutano huo akiwa njiani kurejea jijini Dodoma mara baada ya kumaliza ziara ya siku 4 ya kikazi Mkoani Arusha.


ARUSHA DC

KaziInaendelea✍✍







Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.