Mheshimiwa Penina Mollel ameapishwa rasmi kuwa mjumbe wa Baraza la Mamlaka ya Mji Mdogo Ngaramtoni wakati wa Mkutano wa robo la robo ya pili la Mamlaka hiyo kwa mwaka wa fedha 2017/2018.
Zoezi la kuapishwa kwa mheshimiwa Penina limefanywa na Mkuu wa Kitengo cha Sheria na Usalama Wakili Dustan Shimbo mbele ya wajumbe wa Baraza hilo na kushuhudiwa na watu wote waliokuwepo ukumbini hapo.
Wakili Shimbo amesema kuwa kuanzia sasa Mheshimia Penina Mollel ni mjumbe halali wa Baraza la Mamlaka ya Mji Mdogo Ngaramtoni na anaruhusiwa kufanya shughuli zote za baraza hilo kwa mujibu wa sheria.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.