Na. Elinipa Lupembe.
Katika kipindi cha miaka 4 ya serikali ya awamu ya tano, inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli, serikali imetekeleza miradi mbalimbali kisekta, ikiwemo sekta ya Elimu, Afya, Maji, Nishati na miundombinu ya barabara.
Wananchi wa Kata ya Oljoro halmashauri ya Arusha, wilayani Arumeru ni miongoni mwa wanufaika wa miaka 4 ya serikali ya awamu ya tano, kwa kupata fedha, kiasi cha shilingi milioni 400 za kuboreshwa kwa kituo chao cha Afya Mbuyuni, jambo ambalo ni la kihistoria tangu kupatikana kwa uhuru wa nchi hii, kwa wakazi wa maeneo hayo.
Fedha hizo zimefanikisha ujenzi wa miundombinu ya kituo hicho cha Afya ikiwemo, jengo la Maabara, Jengo la kujifungulia na kulaza mama na mtoto, jengo la Upasuaji pamoja na nyumba ya Mganga.
Tayari kituo hicho kimeanza kutoa huduma, na kinahudumia wananchi wa kata ya Oljoro na vitongoji vyake, wananchi wa wilaya jirani za Monduli na Simanjiro mkoa wa Manyara, huku serikali ikindelea kutoa samani, dawa na vifaa tiba, kuhakikisha kituo hicho kinatoa huduma ya hadhi ya nyota tano.
Shime wananchi wote, tuendelee kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya tano, chini ya uongozi thabiti wa Dkt. John Pombe Magufuli.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.