Na Elinipa Lupembe.
Katika kuendelea kiboresha sekta ya elimu nchini, serikali kupitia Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imeota shilingi milioni 110 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa vituo 5 vya walimu (TRC) vilivyopokea vifaa vya TEHAMA halmashauri ya Arusha.
Mkurugenzi Mtendaji, halmashauri ya Arusha Seleman Msumi, amekiri kupokea kiasi hicho cha fedha ambao tayari kimeingizwa kwenye akaunti za shule vilipo vituo hivyo.
Mkurugenzi Msumi amefafanua kuwa shilingi milioni 110 zitatumika kukarabati vituo vitano huku kila kitio kikigharimu kiasi cha shilingi milioni 22, ikiwa ni utekelezaji wa mradi wa kuimarisha Stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa Elimu ya msingi.
Aidha amevitaja vituo hivyo ni pamoja na Kituo cha walimu Ilkurot kata ya Lengiajve, Mlangarini kata ya Mlangarini, Mringa kata ya Oloirieni, Kambiya Maziwa kata ya Mateves na Naurei kata ya Kiutu.
"Kulingana na maelekezo ya Serikali, mradi huo utatekelezwa kupitia 'Force Account' ikihusisha ukarabati wa majengo ma samani viti na meza 45 kwa kila kitu, na baada ya kukamilika majenga na samani yataandikwa GPE- LANES II". Amefafanua Msumi
Naye Mkuu wa Idara ya Elimu Msingi Mwl. Salvatoru Alute amesema kuwa, mradi huo umekuja wakati muafaka ukiwa ni muendelezo wa kuboresha elimu ukiwapa fursa walimu kujifunza stadi za KKK zitakazowawezesha walimu kukuza taaluma kwa wanafunzi shuleni.
Lengo la serikali kuboresha vituo vya TRC, ni kuhakikisha walimu wanapata elimu wakiwa kazini, inayowajengea uwezo wa kuendeleza mbinu mbalimbali za ufundishaji ili kuwasaidia wanafunzi kujifunza stadi tatu za Kusoma, Kuandika na KuhesKuhe
aARUSHA DC ni Yetu, Tushirikiane Kuijenga"
#Kaziinaendelea ✍✍
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.