• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Milioni 130.4 za TASAF zapunguza adha ya walimu kutembea Kilomita 40 kwenda na kurudi shuleni

Posted on: June 30th, 2018

Na. Elinipa Lupembe.

Jumla ya Miradi miwili ya Elimu iliyotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF imezinduliwa huku mradi mmoja ukitatua changamoto wa walimu kutembea umbali mrefu na kuishi ndani ya eneo la shule na mwingine ukipunguza msingamano wa wanafunzi darasani.

Miradi hiyo ni pamoja na nyumba ya walimu shule ya Msingi Laroi na vyumba viwili vya madarasa, ofisi ya walimu na choo cha wanafunzi, shule ya msingi Themiyasimba kata ya Bwawani.

Miradi hiyo kwa pamoja yenye kugharimu zaidi ya shilingi milioni 130.4, imejenga nyumba ya walimu yenye sehemu mbili kwa shilingi milion 65.7 huku milioni 65.6 zikijenga vyumba viwili vya madarasa, ofisi ya walimu na choo cha wanafunzi.

Mwalimu mkuu shule ya msingi Laroi mwalimu Joyce Kessy amesema kuwa uwepo wa nyumba hiyo ya walimu,licha ya kuwawezesha walimu  kuishi eneo la shule lakini umewapunguzia adha ya kutembea umbali mrefu hadi kufika shuleni hapo kila siku.

Ameongeza kuwa katika eneo hilo hakuna nyumba za kupangisha,  jambo ambalo huwalazimu walimu waliopangiwa shuleni hapo kuishi Jiji la Arusha takribani kilomita Ishirini na hutumia usafiri wa malori ya mchanga kwenda na kurudi.

"Ukosefu wa nyumba za Walimu unawalazimu walimu kuishi mbali, wanaishi kwa Mromboo Kilomita ishirini, usafiri wa kutoka huko ni malori ya mchanga, mvua ikinyesha walimu hulazimika kusubiri mpaka mvua iishe ndipo wafike au watoke shuleni"amethibitisha mwalimu mkuu huyo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, mgeni rasmi na Afisa Elimu Ufundi, Sokoine Mollel, amewataka walimu na wananchi kushirikiana kwa pamoja  kuitunza  miundo mbinu yote iliyojengwa, kwa kuwa, kwa sasa si mali ya serikali bali ni mali ya wananchi hao.

Sokoine ameongeza kuwa, hakuna asiyefahamu adha waliyokuwa wanaipata walimu wanaofundisha shuleni hapo, jambo ambalo huwapa wakati mwingine huwapa, mgumu kuwapanga walimu katika shule hiyo.

"Walimu wanateseka kutembea, huku hakuna nyumba za kupanga, hivyo muwe na uchungu na nyumba hizi, mshirikiane  kuzitunza, kuzishafisha ili zidumu kwa muda mrefu" amesisitiza Sokoine.

Hata hivyo Diwani wa kata ya Laroi, mheshimiwa Ojung Saleko, ameshauri na kuomba ramani za majengo hayo zibadilike ili ziendane na hali halisi ya uhitaji kwa kuwa nyumba hiyo ni kubwa lakini zinaishi familia mbili tu,  wakati ramani ingerekebishwa ingeweza kuwa nyumba ya familia nne.

"Nitoe ushauri kwa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF  kufanya marekebisho ya Ramani za nyumba ambayo kwa gharama hiyo hiyo na ukubwa huo huo unaweza kujenga nyumba ya kuchukua familia nne na si mbili kama sasa.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.