MILIONI 152.4 ZATUMIKAKULIPA KAYA 7,018 ARUSHA DC
Mfuko wa Maendeleo ya Jamii(TASAF) umetumia fedha kiasi cha shilingi milioni 152.4 kuzifikia kaya 7,018 katika utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru KayaMaskini.
Hayo yamesemwa na Mratibu waTASAF Halmashauri ya Wilaya ya Arusha Bi Grace Makema wakati akizungumza nawaandishi wa habari kuhusiana na Zoezi la ugawaji wa fedha hizi walengwa.
Bi Grace Makema amebainishakuwa fedha hizi ni za dirisha la mwezi wa 7 na 8 mwaka 2024 , ikiwa ni malipoya miezi miwili kwa Walengwa na waliohakikiwa kupata kupokea Ruzuku.
“Kipindi hiki tutahakikishahuduma za jamii zinaongezwa na kuboreshwa ili kutoa huduma na kuendelezarasilimali watoto hususan katika upatikanaji wa elimu na afya,”. Amesema Grace.
Amesema TASAF itatekelezamiradi mbali mbali ya Maendeleo kwa wakati na kuzingatia ubora ili iwezekusaidia jamii na kuwa na Maendeleo yaliokusudiwa ,huku ikishirikiana naWananchi wa Maeneo hayo ili jamii kutambua kuwa nao ni sehemu ya Miradi hiyo.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.