Na Elinipa Lupembe.
Jumla ya shilingi milioni 877.9 zimegawiwa kwa walengwa wa Mpango wa kunusu umasikini mradi unaotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii - TASAF na kuzinufaisha Jumla ya kaya 11,159 kwenye vijiji 88 vya halmashauri ya Arusha.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, ofisini kwake, mratibu wa TASAF halmashauri yaArusha, Grace Makema, amesema kuwa kiasi hicho cha fedha kimejumuisha malipo ya awamu mbili ikiwa ni dirisha la 13 la mwazi mwezi Machi na Aprili na dirisha la 14 la mwezi Mei na Juni 2023.
Amefafanua milioni 877.9 zimejuisha fedha za dirisha la 13 ni mlioni 441.3 na milioni 436.58 ni fedha za dirisha la 14.
Hata hivyo ameweka wazi kuwa, kwa mwaka wa fedha uliosha, halmashauri ilitoa ruzuku ya shilingi bilioni 2.5 huku kaya 11,319 zikinufaika.
Aidha ameishukuru serikali ya awamu ya sita kwa mradi huo ambao unawanufaisha wananchi wasio na wenye uwezo mdogo kiuchumi, mpango ambao unaendeleza mapambano dhidi ya adui ujinga, umasikini na maradhi nchini,
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.