Na. Elinipa Lupembe.
Wajumbe wa Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango, halmashauri ya Arusha, wametembelea na kukagua miradi ya maendeleo yenye thamani ya shilingi bilioni 1.2 katika sekta ya Elimu, Afya na mifugo pamoja na maeneo ya wazi katika sekta ya ardhi.
Wajumbe hao wamefanikiwa kupitia na kukagua jumla ya miradi 9 na kuridhishwa na utekelezaji wa miradi 7 hiyo ya maendeleo, inayotekelezwa ndani ya halmashauri ya Arusha kwa kipindi cha robo ya tatu kwa mwaka huu wa fedha uanoendelea 2021/2022.
Akizungumza wakati wa kikao cha majumuisho ya ziara hiyo Makamu Mwenyekiti wa halmashauri, Mheshimiwa Freddy Lukumay, amesema kuwa, kamati imeridhishwa na ubora wa miradi ya ujenzi, unaokwenda sambamba na thamani ya fedha za miradi zilizotolewa na serikali ya awamu ya sita.
Aidha amewapongeza watalamu wa halmashauri wa ngazi zote, viongozi wawakilishi wananchi pamoja na wananchi kwa umoja wao, unaowezesha utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika maeneo yote ndani ya halmashauri.
."Tunawapongeza watalamu wa ngazi zote, miradi tuliyotembelea ni mizuri, tunaona ushiriki wa viongozi wa ngazi zote pamoja na wananchi, ushiriki wa watalamu pia, hii inaongeza uwazi na ukweli pamoja na hali yaa umiliki wa miradi kwa wananchi wetu" amesema Makamu Mwenyekiti huyo.
Hata hivyo wajumbe hao wameagiza uongozi wa halmashauri, kusimamia kasi ya ujenzi wa miradi yote na kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati kulinga na mikataba ya wakandarasi husika, na kuagiza pia kuendelea kuyapima maeneo yote yanayomilikiwà na halmashauri pamoja na kuendelea kuyatambua maeneo yote ya halmashauri.
Naye Mkurugenzi Mtendaji, halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi, ameahidi kuendelea kusimamia utekelezaji wa miradi hiyo kwa kuwabana wakandarasi wote, kumaliza miradi kwa wakati kulingana na mikataba yao, lengo likiwa ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma kulinga na matarajio ya serikali yao.
Aidha ameitaja miradi 9 iliyokaguliwa yenye thamani ya shilingi bilioni 1,2, ni pamoja na ujenzi wa nyumba 3 za wakuu wa idara na vitengo mradi uliogharimu shilingi milioni 150, ujenzi wa shule mpya ya sekondari Olomitu kwa shilingi milioni 60, ujenzi wa shule mpya ya msingi ya mchepuo wa kiinggereza Samia Suluhu Hassan Academy kwa shilingi milioni 250, ujenzi wa kituo kipya cha afya Oloirieni milioni 450 na upanuzi wa kituo cha afya Oldonyosambu kwa shilingi milioni 300.
Msumi ameyataja maeneo ya wazi yanayomilikiwa na halmashauri ni pamoja na maeneo ya mifugo kata ya Kiranyi na Kimyaki pamoja na jengo la halmashauri lililoko eneo la Engira Road Jijini Arusha.
"Vyanzo vya fedha zilizotumika kutekeleza miradi yote ya ujenzi ni pamoja na fedha kutoka serikali Kuu na fedha za mapato ya ndani kupiti fidia ya deni la shamba la Lakilaki"amefafanua Mkurugenzi Msumi
Ziara hiyo ya Kamati ya fedha ni ya kawaida yenye jukumu lamkukagua shughuli za utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya halmasahuri kwa kila robo ya mwaka,myaani kila baada ya miezi mitatu.
ARUSHA DC
#KaziInaendelea ✍✍
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.