• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Mkakati wa kudhibiti mbwa kuzaliana watekelezwa Arusha DC

Posted on: March 12th, 2018

Madaktari wa mifugo halmashauri ya Arusha wilayani Arumeru,  wameanza mkakati wa kuthibiti mbwa kuzaliana kwa kuwafaniyi upasuaji wa kuhasi mbwa dume na kuwatoa vizazi mbwa jike kwa lengo la kupunguza mbwa wanaozurura mitaani na kuwa kero kwa wakazi..

Akizungumza na mwandishi wetu,  daktari wa mifugo halmashauri ya Arusha, Dkt. Yohana Kiwone, amesema kuwa zoezi hilo ni la kawaida kufanyika kwa mifugo aina ya mbwa ambao kwa kawaida huzaliana kwa wingi na kutokuwa na faida yoyote kwa jamii, zaidi ya kuchafua mazingira na kusababisha kero kubwa kwa jamii.

Dkt. Kiwone amesema kuwa wamefanya zoezi hilo katika kitongoji cha Meriti kata ya Iliboru na kufanikiwa kufanya upasuaji wa kuhasi jumla ya mbwa dume kumi  na kutoa vizazi 'ovario-hysterectomy' mbwa jike wawili.

Amefafanua kuwa zoezi hilo la kuhasi ni njia mojawapo ya kupunguza uzalianaji holela wa mbwa wasiokuwa na kazi na kupunguza tatizo la mbwa wanaozurura mitaani ambao ni kero kwa jamii.

Ameongeza kuwa mbwa wanaozurura licha ya kuwa ni kero lakini pia ni hatari sana kwa afya ya binadamu kutokana na mbwa hao kutokupatiwa chanjo wala tiba yoyote, jambo ambalo linaweza kusababisha maambukizi ya magonjwa ya mbwa kwa binadamu.

Dkt. Kiwone ameelezea madhara yanayotokana na mbwa wazururaji ni pamoja maambukizi ya ugonjwa wa kichaa cha mbwa kwa binadamu ugonjwa unaosababishwa na mbwa hao kutokupata chanjo ya ugonjwa huo, pamoja na uharibifu unaotokana na wizi wa mbwa unaosababisha hasara kwenye jamii.

" Mbwa anayezurura hapati chanjo wala tiba yoyote, akimng'ata mtu obvious mtu yule atapata maambukizi ya magonjwa ya mbwa huyo, pengine ugonjwa wa kichaa cha mbwa ambao mtu asipopata matibabu kwa haraka anaweza kupoteza maisha na matibabu yake ni ghali pia" amesema Dkt. Kiwone

John Laizer mkazi wa Ilboru amepongeza zoezi hilo kwa kuthibitisha kero ya mbwa wazururaji katika eneo lao na kusema kuwa, mbwa hao wananchafua mazingira na pia ni wezi wa vyakula na mifugo hasa kuku na mayai katika nyumba zao.

" Mbwa hawa wanatukera sana, ukisahau kidogo kufunga milango, huna bahati.., mbwa anaingia ndani na kuiba kama ni chakula, kama ni kuku kwenye banda, kiukweli wanasababishia watu hasara, tunaishi kwa hofu ya kuibiwa na mbwa, mbwa hao wamekua sio walinzi tena bali ni wezi " amesema Laizer

Hata hivyo Dkt. Kiwone amewataka wafugaji wa mbwa kuthibiti mbwa kuzaliana kwa kuwahasi na kuwatoa vizazi ili kufuga mbwa wanaoweza kumudu kuwatunza na kuepuka kero na madhara yanayoweza kuwapata binadamu kutokana na mbwa wazururaji wasiotunzwa.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.