Kuelekea kwenye maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike duniani itakayoadhimishwa kesho, walimu wa shule zote za Msingi Halmashauri ya Arusha wilayani Arumeru wametakiwa kutumia muda walau wa dakika 40 kuzungumza na watoto wa kike juu ya haki, wajibu, pamoja na kujitambua thamani yao na kutoa taarifa pindi wanapofanyiwa matukio ya ukatili na mtu yoyote, mazungumzo yatakayofanyika katika madarasa yao kwenye shule zao.
Maagizo hayo yametolewa na Afisa Elimu Msingi Halmashauri ya Arusha mwalimu Tumsifu Mushi wakati alipokutana na Waratibu wa Klasta, Maafisa Elimu Kata na walimu wakuu wa shule Msingi za serikali za halmashauri hiyo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Shule ya Green Acres na kujadili changamoto zinazowakabili watoto wa kike katika halmashauri ya Arusha.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.