• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA JELA KWA KUMBAKA NA KUMLAWITI MTOTO WA MIAKA 9.

Posted on: July 19th, 2022

 Na Elinipa Lupembe

Mahakam ya Wilaya ya Arumeru  mkoani Arusha imemhukumu kifungo cha miaka 30 na kifungo cha maisha jela, Bw. Fadhili Sumaiyani  mwenye umri wa miaka 30, mkazi wa Kitongoji cha Seuri, Kata ya Olturumet  halmashauri ya Arusha kwa kosa la kumbaka na kumlawiti mtoto wa miaka tisa.

Akitoa hukumu hiyo Julai 19, 2022 Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya wilaya, Gwantwa Mwankunga,  amesema kuwa, Mahakama hiyo imefikia uamuzi huo, mara baada ya kujiridhisha na ushahidi uliotolewa pasipo na shaka yoyote na kumtia hatiani mtuhumiwa huyo kwa makosa mawili la kubaka na kulawiti.

Hakimu huyo amemtianhatiani kwa kosa la kubaka chini ya kifungu na 154 na kosa la kubaka chini ya kifungu cha 130 na 131 vya kanunia ya adhabu.

Mwendesha mashitaka na Wakili wa Serikali Liliani Mmasi, aliieleza mahakama hiyo kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo mnamo tarehe 19 Mei, 2021 katika Kitongoji cha Seuri, kwenye eneo analofanyia kazi ya ulinzi mtuhumiwa, ambapo alimbaka na kumlawiti  mtoto huyo wa miaka tisa mwanafunzi wa darasa la tatu, na kumsababishia maumivu makali.

Muendesha mashtaka huyo, amefafanua kuwa, mtuhumiwa alimbaka na kumlawiti  mtoto huyo majira ya saa 11 jioni,  wakati mtoto huyo akielekea dukani, alikokuwa ametumwa na mama yake kununua mahitaji ya nyumbani, katika eneo ambalo mtuhumiwa anafanya kazi ya kulinda nyumba ambayo haijakamilika ujenzi.

Aidha Mwendesha mashitaka, aliiomba mahakama itoe adhabu kali kwa mtuhumiwa kwa makosa yote mawili, ili iwe ni fundisho kwa watu wengine wenye nia ovu ya kutaka kufanya vitendo kama hivyo kwa watoto.

Upande huo wa mashitaka uliwasilisha mashahidi watano  ambao pasipo kuacha shaka yoyote mahakama ilimkuta mtuhumiwa na makosa mawili, na kuamua kumtia hatiani kwa kumfunga kifungo cha miaka thelathini kwa kosa la kubaka na kifungo cha maisha kwa kosa la kulawiti, na kutumikia adhabu zote mbili kwa pamoja huku adhabu kubwa ikibeba adhabu ndogo.

Awali mkurugenzi wa shirika la lisilo la kiserikali CWCD, Hindu Mbwega, ameishukuru mahakama kwa kumtia hatiani mtuhumiwa huyo, kutokana na kukithiri kwa vitendo vya ukatili kwa watoto, na kuionya kuacha kufanya vitendo hivyo huku akiitaka jamii kuwafichua watu wanaofanya vitendo vya ukatili kwa watoto na kuwasisitiza watu wenye nia ovu kutambua kuwa sheria inafanya kazi kwa yeyote atakayejihusisha na vitendo hivyo.

Naye Afisa Ustawi wa Jamii, halmashauri ya Arusha, Josina Mlaki ameweka wazi kuwa, licha ya kuwa serikali kwa kushirikiana na ASAS za kiraia wanatoa elimu kwa jamii juu haki za mtoto pamoja na kumlinda mtoto dhidi ya vitendo vya ukatili lakini bado kuna changamoto ya jamii kukosesha watoto haki zao, kwa kukataa kutoa ushahidi na kusababisha baadhi ya kesi  kushindwa kuwatia hatiani watuhumiwa huku wakiwa wamefanya makosa hayo kwa watoto.

Tafiti zinaonesha kuwa asilimia 75 ya vitendo vya ukatili kwa watoto nchini, vinafanywa na watu wa karibu ndani ya familia na jamii zinazowazunguka watoto.


ARUSHA DC

KaziIendelee✍✍

JIANDAE KUHESABIWA



Bw. Fadhili Sumaiyani  mwenye umri wa miaka 30, mkazi wa Kitongoji cha Seuri, Kata ya Olturumet  halmasahuri ya Arusha amehukumiwa kifungo cha maisha kwa kosa la kumbaka na kumlawiti mtoto wa miaka tisa.







Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.