Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha Ndg Seleman Msumi amewakaribisha wawekezaji kote Nchini na Nje ya Nchi kuja kuwekeza, Halmashauri hapa kwakuwa kuna fursa nyingi za uwekezaji na maeneo mengi yanapatikana.
Bw Seleman Msumi ameyasema hayo hii leo alipotembelea banda la Halmashauri ya Wilaya ya Arusha, kwenye maonesho ya wakulima na wafugaji ya Nane Nane Kanda ya Kaskazini kusini, mkoani Arusha.
Akizitaja baadhi ya fursa za uwekezaji ambazo wadau wanweza kuwekeza ni uwekezaji kwenye kilimo, ufugaji, viwanda na sekta nyingine, kwani Halmashauri imeshatenga Maeneo uwekezaji ambao utakuwa na Tija Kwa Halmashauri na Taifa Kwa Ujumla.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.